Nyigu-kekeo (Chrysididae)
Nyigu-kekeo | ||||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Nyigu-zumaridi (spishi isiyotambuliwa)
| ||||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||||
Makabila 5:
|
Nyigu-kekeo au nyigu-zumaridi (kutoka kwa Kiing. cuckoo wasps au emerald wasps) ni nyigu wadogo wa nusufamilia Chrysidinae katika familia Chrysididae ya oda Hymenoptera walio na rangi zinazong'aa kama johari, k.m. kijani, buluu na nyekundu. Nyigu hawa hawachomi. Kama vile kekeo, majike hutaga mayai yao katika viota vya nyuki na nyigu wapweke, ambayo ni asili ya jina lao la kwanza. Walipata jina lao la pili kwa sababu spishi za kwanza zilizojulikana sana zilikuwa kijani kama zumaridi kabisa au kwa sehemu kubwa. Spishi zilizo na fumbatio nyekundu huitwa nyigu mkia-yakuti pengine (jina lisilo sahihi sana).
Maelezo
[hariri | hariri chanzo]Hawa ni nyigu wadogo wenye urefu wa mm 3-22, ingawa mara chache huzidi mm 12. Wana kiunzi nje kigumu sana. Pingili tatu tu zinaonekana kwenye fumbatio[1]. Mabamba ya mgongo ya pingili hizi hujipinda na kuficha mabamba ya tumbo zisionekane kutoka upande. Mabamba ya tumbo ni bapa au mbonyeo[2]. Pingili nyingine zimerudishwa ndani ya mwili na kuunda neli za uzazi. Neli ya kutagia hutumika tu kwa kutaga mayai na sio kwa kuchoma[3]. Nyigu-kekeo wana rangi angavu, haswa kijani, buluu na nyekundu, ambazo hutokea peke yao au kwa michanganyiko. Zinang'aa kama zumaridi, zabarijadi na yakuti.
Biolojia
[hariri | hariri chanzo]Nyigu-kekeo ni vidusia wa nyigu na nyuki wapweke[3]. Majike huingia katika mashimo ya viota ambapo hutaga yai karibu na kila yai au buu la kidusiwa. Kisha buu anayeibuka hula buu kidusiwa au, katika spishi nyingine, kwanza buu kidusiwa akiwa bado mdogo, na kisha chakula kilichotolewa na mdudu kidusiwa[3]. Jike hulindwa dhidi ya kidusiwa aliyekasirika kwa kiunzi nje kigumu na kwa tabia yake ya kujiviringa katika tufe ili kulinda miguu yake na sehemu za chini za kichwa[4].
Spishi za Afrika ya Mashariki
[hariri | hariri chanzo]
|
|
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Chrysis angolensis
-
Chrysis bicolor
-
Chrysis chrysostigma
-
Chrysis fulgida
-
Chrysis ignita
-
Chrysis smaragdula
-
Hedychrum nobile
-
Stilbum cyanurum
-
Stilbum cyanurum aliyejiviringa katika tufe
-
Trichrysis cyanea
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Torretta, J.P. (2015). "Host–parasite relationships and life cycles of cuckoo wasps in agro-ecosystems in Argentina (Hymenoptera: Chrysididae: Chrysidini)". Journal of Natural History. 49 (27–28): 1641–1651. doi:10.1080/00222933.2015.1005710. S2CID 84594440.
- ↑ Lucena, D.; Kimsey, L.S.; Almeida, E. (2019). "Phylogenetic relationships and biogeography of the Ipsiura cuckoo wasps (Hymenoptera: Chrysididae)". Systematic Entomology. 44 (1): 192–210. doi:10.1111/syen.12320. S2CID 92508094.
- ↑ 3.0 3.1 3.2
Kimsey, L.S. (2006). "California cuckoo wasps in the family Chrysididae (Hymenoptera)".
{{cite journal}}
: Cite journal requires|journal=
(help) - ↑ Triplehorn, C.A.; Johnson, N.F.; Borrow, D.J. (2005). Borrow and DeLong's Introduction to the Study of Insects.