Nenda kwa yaliyomo

Nyamko Sabuni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nyamko Sabuni, Uswidi (2011)

Nyamko Ana Sabuni (amezaliwa 31 Machi 1969) ni mwanasiasa nchini Uswidi aliyechaguliwa kuwa waziri katika serikali ya Fredrik Reinfeldt tangu Oktoba 2006. Anasimamia wizara ya kuingiza katika jamii wahamiaji waliofika Uswidi pamoja na usawa wa kijinsia.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Nyamko Sabuni alizaliwa mjini Bujumbura katika Burundi. Wazazi walikuwa wakimbizi wa kisiasa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakaendelea kupata kimbilio Uswidi mwaka 1981. Hivyo Nyamko alifika Uswidi alipokuwa na umri wa miaka 12.

Baada ya kumaliza shule alianza kusoma sheria, nadharia ya uhamiaji na mawasiliano kwenye chuo kikuu.

Mwaka 1996 alijiunga na kitengo cha vijana cha chama cha liberal akaendelea kuchaguliwa mbunge mwaka 2002.

Bungeni alipigania haki za wahamiaji, hasa wa kinamama na wasichana. Alidai utafiti wa kiganga kwa mabinti wote wa shule kwa kusudi la kuzuia kukeketwa kwa wasichana kutoka familia za wahamiaji wanaoleta desturi hii marufuku kutoka utamaduni wao.[1]

Alidai pia sheria ya kupiga marufuku kuvaliwa kwa hijabu shuleni kwa mabinti walio chini ya umri wa miaka 15.

Alipendekeza pia sheria mpya itakayoweka adhabu za pekee kwa mauaji wa mabinti na wanawake kutokana na dhana ya kuchafuliwa kwa heshima ya familia.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. 'Check all schoolgirls for circumcision' The Local, 17 Julai 2006.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]