Nronga
Nronga ni kijiji cha kata ya Machame Magharibi katika Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania Kaskazini Mashariki.
Kijiji cha Nronga ni miongoni mwa vijiji vichache katika mkoa wa Kilimanjaro vinavyopakana na Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro. Kaskazini mwa kijiji hicho ndipo msitu mkubwa wa hifadhi hiyo unapopatikana.
Kijiji hicho ni kama kisiwa kwa sababu kimezungukwa na mito miwili mikubwa inayotiririsha maji yake kutoka kwenye mlima Kilimanjaro.
Upande wa mashariki kuna mto mrefu unaoitwa Kikafu na kwa upande wa magharibi kuna mto unaoitwa Semira na mito hiyo inaungana au kukutana karibu kabisa na daraja au lango la kuingilia kwenye kijiji hicho.
Hali ya hewa ni nzuri sana na ya baridi, tena mvua za kila mara zinazonyesha huko zinafanya kijiji kiwe na mazingira mazuri ya ujani yanayovutia na kupendeza macho.
Watu na wakazi wa kijiji hicho wanajishughulisha na kilimo cha kahawa, ndizi na mazao mengine kama mahindi na maharage. Hivyo uchumi wa kijiji unategemea sana kilimo pamoja na ufugaji.
Huko mwandishi Elieshi Lema alizaliwa mwaka 1949.
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Nronga kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
|