Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro

Kilele cha Mawenzi cha Mlima Kilimanjaro
Mahali pa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro
MahaliMkoa wa Kilimanjaro, Tanzania
Nearest cityMoshi
Eneo753 km² (291 mi²)
Kuanzishwa1973
Lango la Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro.

Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro ni hifadhi ya taifa nchini Tanzania, lakini ni maarufu duniani kutokana na mandhari mazuri ya Mlima Kilimanjaro ambao ni mlima mrefu kuliko yote barani Afrika na unapatikana katika nchi ya Tanzania.

Hifadhi hii ina ukubwa wa kilometa za mraba 755 na iko umbali wa kilometa 45 kutoka Moshi mjini, kusini mwa Mkoa wa Kilimanjaro, 2 ° 50'-3 ° 10'S latitude, 37 ° 10'-37 ° 40'E longitude.

Hifadhi hiyo inajumuisha Mlima Kilimanjaro inayozungukwa na ukanda wa msitu wa mlimani ulio mita 1,820 (futi 5,970).

Kilele cha Kibo, chenye urefu wa mita 5895 (futi 19340), ndicho kivutio kikubwa kwa wageni kutoka ndani na nje ya nchi kwa sababu ya kufunikwa na theluji mwaka mzima.

Mlima huu ni moja kati ya milima ambayo kilele chake hufikiwa kwa urahisi na hivyo kuwa kivutio kikubwa kwa wapanda milima kutoka kila pande za dunia.

Safari ya kupanda mlima huu humpitisha mpandaji katika kanda za hali ya hewa tofauti kuanzia ile ya nchi za tropiki hadi aktiki.

Zaidi ya watalii 20,000 hupanda mlima huu kila mwaka wakiwemo wageni kutoka nje ya nchi na Watanzania. Mpandaji wa mlima huu huhitaji angalau siku tano, siku tatu kupanda na siku mbili kuteremka.

Kuna njia sita za kukwea mlima Kilimanjaro hadi kileleni.

Njia iliyo rahisi na maarufu zaidi ni ile ya kuanzia lango la Marangu, ambako ndiyo makao makuu ya hifadhi. Njia njingine ya kupandia mlima ipo Tarakea (Rombo).

Wanyama kadhaa hupatikana katika msitu unaozunguka Mlima Kilimanjaro wakiwemo mbega, nyani, nyati, chui, tembo, swala na ndege mbalimbali.

Hifadhi inasimamiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa ya Tanzania (TANAPA).

Wakati mzuri wa kutembelea hifadhi[hariri | hariri chanzo]

Kuanzia mwezi Desemba hadi Februari, na pia Julai na Septemba (ingawa wakati huo ni baridi zaidi).

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Majarida ya hifadhi za Taifa Tanzania

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Flag-map of Tanzania.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Isipokuwa usitaje majina ya viongozi waliopo sasa maana wanabadilika haraka mno.