Marangu
Marangu ni mji ulioko katika Wilaya ya Moshi Vijijini, Mkoa wa Kilimanjaro.
Neno "Marangu" linamaanisha mahali penye vijito vingi vya maji. Mji huu ni kati ya maeneo maarufu nchini Tanzania.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Kabla ya uhuru mwaka 1961, mji wa Marangu ulikuwa makao makuu ya wilaya ya Vunjo iliyokuwa chini ya (Mangi Mwitori) Petro Itosi Marealle na (Mangi Mkuu) Thomas Marealle, aliyepewa ufalme mwaka 1951, ambaye aliishi katika mji wa Moshi.
Uchumi
[hariri | hariri chanzo]Wakazi wengi wa Marangu ni wakulima wa ndizi, mboga za majani na kahawa. Hata hivyo, chanzo kikuu cha mapato ni utalii kutokana na Mlima Kilimanjaro na vivutio vingine.
Elimu
[hariri | hariri chanzo]Shule mbalimbali na vyuo, kama vile Chuo cha Ualimu cha Marangu na Shule ya Wasichana ya Ashira, viko katika mji huu vikitoa huduma kwa wanafunzi toka maeneo mbalimbali ya Tanzania.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Marangu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
|