Thomas Marealle

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Thomas Marealle

Chifu Thomas Lenana Marealle II (Juni 15 1915 - Februari 14 2007) alikuwa Chifu Mkuu (Mangi Mkuu) wa Kabila la Wachaga nchini Tanzania na mwanasiasa.

Baada ya kushinda uchaguzi mkuu wa uchifu, ambao alishindana na Abdi Shangali wa Wilaya ya Hai, Jackson Kitali wa Moshi, Petro Marealle wa Vunjo na John Maruma wa Rombo, Chifu Mareale alitawazwa kuwa chifu Januari 1952. Thomas Marealle alitawala pamoja na Chifu Mangi Mwitori. Petro Itosi Marealle Kuimarisha mamlaka kutoka kwa machifu wengine 3 wa Wachaga hivyo kuwafanya Wachaga kuwa na nguvu zaidi na kudhibiti mambo yao wakati wa ukoloni. Serikali ilifuta mfumo wa Uchifu mwaka 1961, ingawa Marealle, akitarajia hili, aliacha wadhifa wake kwa hiari mwaka uliotangulia. Muda wake kama Mangi Mkuu ulionekana kuwa wakati mzuri, ulioangaziwa na maboresho makubwa ya elimu, afya, harakati za ushirika na mawasiliano katika eneo lake. Hasa mfumo wake wa mahakama na mfumo wake wa ugawaji wa maji sawa unakumbukwa kwa hamu kubwa. Baada ya kufanya kazi kwa [[Umoja wa Mataifa] katika uwanja wa misaada ya kigeni kwa miaka kumi na tatu, alistaafu kama mwanadiplomasia. Alifariki tarehe 14 Februari 2007 akiwa na umri wa miaka 92, na kuzikwa nyumbani kwao Marangu, Moshi.[1]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Chief Marealle II: Man who "educated" Kilimanjaro", IPP Media, 2007-02-28. Retrieved on 2007-08-03. Archived from the original on 2007-03-03. 
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Thomas Marealle kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.