Noela Rukundo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Noela Rukundo ni mwanamke mwenye uraia pacha wa Burundi-Australia ambaye alijulikana baada ya kuaminika amekufa na kujitokeza siku ya mazishi yake mwenyewe. Mnamo Januari 2015, alidhaniwa kuwa amekufa baada ya mumewe, Balenga Kalala kuwalipa kwa siri watu kadhaa wenye silaha ili wamuue alipokuwa Burundi kwa mazishi ya mama yake wa kambo. Hata hivyo, bila kufahamu mumewe Bwana Kalala, watu hao wenye silaha walikataa kumuua Bi.Rukundo, ingawa walimweleza kuwa wamemwua. Walimwachilia siku mbili baadaye na kumpa ushahidi wa kumshtaki mumewe kwa mipango yake ya kumuua. Kufuatia mazishi ya Rukundo mwenyewe Februari 2015, ambapo Kalala aliwaambia waliohudhuria kuwa aliuawa katika ajali mbaya, laini Rukundo alifika nyumbani walipokuwa wakiishi wanandoa hao huko Australia bila kutangazwa na kumkabili mumewe. Baadaye Kalala alishtakiwa kwa uchochezi wa mauaji na kuhukumiwa kifungo cha miaka tisa jela.[1]

Historia kwa Ufupi na Jaribio la Mauaji yake[hariri | hariri chanzo]

Noela Rukundo alihama kutoka Burundi hadi Australia kama mkimbizi mnamo mwaka wa 2004, akiwa ni mama wa watoto watano kwa wakati huo.[2] Muda mfupi baadaye alikutana na Balenga Kalala ambaye alilkuwa ni opareta wa forklift na mkimbizi kutoka nchini Kongo ambaye pia alikuwa amewasili mwaka wa 2004 kukimbia jeshi la waasi ambalo lilikuwa limeua mke na mtoto wake alipokuwa na umri wa miaka 24.[3] Wawili hao walishirikiana na mfanyakazi wa shughuli za kijamii katika wakala wa makazi mapya ambapo walienda wote wawili ambaye mara nyingi alimwomba Kalala ambaye alizungumza Kiingereza kumsaidia kutafsiri Rukundo ambaye alizungumza Kiswahili.[4] Wawili hao walianza uhusiano na wakahamia pamoja katika kitongoji cha Kings Park cha Melbourne na haraka wakafunga ndoa na kupata watoto watatu pamoja.[5]

Mumewe Bwana Kalala alianza kushuku kuwa Rukundo alikuwa akimsaliti kimapenzi na mwanaume mwingine na akalipa karibu dola 7,000 kwa kundi la watu wenye silaha ili kumuua. Tarehe 21 Januari 2015, Rukundo akiwa hotelini jijini Bujumbura kuhudhuria mazishi ya mama yake wa kambo nchini Burundi alizungumza na Kalala kwa simu ambaye alimuagiza atoke nje ili apate hewa safi. Karibu mara tu baada ya kutoka nje ya hoteli yake alikabiliwa na mtu akiwa amenyooshewa bunduki na kumlazimisha kuingia ndani ya gari ambako kulikuwa na wanaume wengine wawili wenye silaha waliokuwa wakingoja ndani ya gari hilo.[6] Walimfunga macho na kitambaa na kumpeleka kwenye ghala la mashambani ambako alifungwa kwenye kiti.[7][8] Wakiwa huko mtu wa nne kati ya wale wauaji alifichua kuwa Kalala aliamuru wamuue lakini hawatafanya hivyo kwa vile wanamfahamu kaka yake na Rukundo na walikataa kuua wanawake na watoto. Ingawa mwanzoni hakuamini kwamba mumewe alijaribu kumuua, watekaji nyara walimthibitishia hilo kwa kumpigia Kalala kwa simu ya mkononi na kuweka sauti ya spika ya nje ambayo rukundo alisikia kwa masikio yake. Katika simu hiyo alithibitisha kwamba alitaka afe, jambo ambalo lilimfanya Rukundo kuzimia.[2]

Wale watu wenye silaha (wauaji waliokodiwa) walimweleza Rukundo kwamba wangehifadhi zile pesa walizopewa na Kalala mwanzoni, na wamwambie kwamba wamemuua tayari ili waweze kupata kiasi chao kilicho bakia ambazo zilikuwa dola za kimarekani 3,400 zaidi baada ya kumaliza kazi hiyo kikamilifu.[2] Wakati huo Rukundo alikuwa bado hajapatikana na kaka yake ambaye pia alikuwa Burundi alianza kuwa na wasiwasi.[4] Alimpigia simu shemeji yake Kalala na kumwomba atume dola 545 ili polisi wafanye uchunguzi wa kutoweka kwake ambapo Kalala alituma. Mnamo tarehe 19 Februari, watekaji nyara walimshusha Rukundo kando ya barabara wakiwa na bahasha iliyojaa ushahidi wa kumshtaki Kalala ikiwa ni pamoja na rekodi za mazungumzo ya simu naye akipanga mauaji ya Rukundo pamoja na risiti mbili kutoka Western Union za malipo ya dola 7,000.[9][10]Pia walimwambia Rukundo kwamba alikuwa na saa 80 za kuondoka nchini humo.[11]

Kumkabili Mumewe na Matokeo yake[hariri | hariri chanzo]

Huko Melbourne, Kalala alitayarisha mazishi ya Rukundo ambaye aliwaambia watu wa jumuiya ya Kiafrika huko Melbourne, kwamba mkewe amefariki katika ajali mbaya. Wakati huo Rukundo aliwasiliana na balozi za Kenya na Ubelgiji ili kumsaidia kuweza tena kurudi Melbourne. Pia alimpigia simu kasisi wa kanisa lake huko Melbourne ambaye alimweleza kwamba bado yupo hai na kumwomba msaada. Baada ya kurejea Melbourne tarehe 22 Februari, alifika nyumbani kwake ambapo kundi la mwisho la waombolezaji walikuwa wametoka tu kwenye mazishi yake. Alipotoka kwenye gari Kalala aliweka mikono kichwani huku akionekana kuwa ni mtu mwenye kujawa na hofu. Aliuliza, "Je, ni mzimu?" Alimgusa bega ili kuona kama ni kweli alikuwa mwenyewe na akaruka alipogundua kuwa alikuwa Rukundo akajibu, "Ajabu! Mimi bado ni hai!" Kalala alipiga mayowe na kuanza kuomba radhi sana kwa Rukundo ambaye aliwapigia simu polisi.

Baada ya kupata amri ya mahakama dhidi yake, polisi walirekodi kwa siri mazungumzo kati yake na Rukundo ambapo alimwomba msamaha na kukiri kuwa ni kweli yeye aliratibu jaribio hilo la mauaji ya Rukundo.[4] Baada ya kukamatwa Kalala alikana kuwa yeye hakuhusika kuamuru Rukundo auawe. Hata hivyo baadaye polisi walipeleka ushahidi wa sauti yake iliyorekodiwa kwa siri akikiri kuwakodisha watu wenye bunduki ili wamuue kewe alianza kulia.[12] Maelezo yake ya kujaribu kufanya Rukundo auawe yalikuwa ni kwamba "wakati fulani [shetani] anaweza kuingia ndani ya mtu kufanya jambo fulani".[13] Tarehe 11 Desemba 2015, Kalala alishtakiwa na mahakama ya Melbourne kwa uchochezi wa mauaji, na kuhukumiwa kifungo cha miaka tisa jela na kwa sheria za nchini humo atastahiki parole mwaka wa 2022.[14] Watu wa jamii ya Kongo walimtisha Rukundo kwa kuripoti Kalala. [11]

Umaarufu wake Katika utamaduni[hariri | hariri chanzo]

Tukio hili liligeuka fursa kwa watengeneza filamu mnamo mwaka 2021 kampuni ya filamu ya Lifetime ilitengeneza filamu ya Death Saved My Life, kuhusu mwanamke anayeitwa Jade (iliyoigizwa na Meagan Good) ambaye alidanganya kifo chake baada ya mumewe mnyanyasaji kukodi jambazi amuue,filamu hii ilitokana na hadithi ya Rukundo.[15] Pia mnamo 2021, video ya mtandao wa kijamii wa TikTok kuhusu hadithi ya Rukundo ilisambaa sana mtandaoni.[16]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. "Spared by the hitmen with principles", BBC News (kwa en-GB), 2016-02-05, iliwekwa mnamo 2022-03-17 
 2. 2.0 2.1 2.2 "Woman forgives husband who paid hit men to kidnap, murder her in Africa", ABC News (kwa en-AU), 2015-12-11, iliwekwa mnamo 2022-03-17 
 3. "Woman forgives husband who paid hit men to kidnap, murder her in Africa", ABC News (kwa en-AU), 2015-12-11, iliwekwa mnamo 2022-03-17 
 4. 4.0 4.1 4.2 "Spared by the hitmen with principles", BBC News (kwa en-GB), 2016-02-05, iliwekwa mnamo 2022-03-17 
 5. "Wife crashes her own funeral, horrifying her husband, who had paid to have her killed", Washington Post (kwa en-US), ISSN 0190-8286, iliwekwa mnamo 2022-03-17 
 6. Mark Russell (2015-11-17). "'Surprise! I'm still alive': wife confronts man who paid to have her killed". The Age (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-03-17. 
 7. "Wife Who Crashed Her Own Funeral To Spite Murderous Husband Has One Inspirational Message". HuffPost UK (kwa Kiingereza). 2016-02-05. Iliwekwa mnamo 2022-03-17. 
 8. "Woman forgives husband who paid hit men to kidnap, murder her in Africa", ABC News (kwa en-AU), 2015-12-11, iliwekwa mnamo 2022-03-17 
 9. "Her husband thought he had her killed, so she crashed her own funeral". www.washingtonpost.com. Iliwekwa mnamo 2022-03-17. 
 10. Mark Russell (2015-11-17). "'Surprise! I'm still alive': wife confronts man who paid to have her killed". The Age (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-03-17. 
 11. 11.0 11.1 Evann Gastaldo. "Woman crashes own funeral after husband's murder plot". USA TODAY (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2022-03-17. 
 12. https://www.cbc.ca/news/trending/woman-funeral-murder-confront-1.3436832
 13. "Woman turns up at her own funeral and shocks the husband who paid to kill her". www.telegraph.co.uk. Iliwekwa mnamo 2022-03-17. 
 14. https://www.washingtonpost.com/video/national/wife-describes-crashing-her-own-funeral/2016/02/05/fb40196e-cc1a-11e5-b9ab-26591104bb19_video.html
 15. "'Death Saved My Life' Is Based On A Jaw-Dropping True Story Of A Faked Death". Bustle (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-03-17. 
 16. "TikToker Shares True Story About Time A ‘Dead’ Woman Appeared At Her Own Funeral". www.unilad.co.uk (kwa Kiingereza). Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-03-17. Iliwekwa mnamo 2022-03-17. 
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Noela Rukundo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.