Nemesiani na wenzake

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Nemesiani na wenzake Feliche, Lucho, Feliche, Liteo, Poliano, Vikta, Iader na Dativus (walifariki 258 hivi) walikuwa maaskofu ambao, pamoja na mapadri, mashemasi na waumini wengine wa Numidia (eneo la Algeria ya leo), walipelekwa Sigum kufanya kazi ya shokoa katika migodi wakifia hivyo dini ya Ukristo chini ya kaisari Valerian[1].

Sipriani mfiadini, askofu mkuu wao, aliwaandikia barua ya kuwatia moyo pamoja na kuwatumia misaada, nao walijibu barua tatu kutoka sehemu tofauti.

Tangu kale wanaheshimiwa na Waorthodoksi wa Mashariki, Waorthodoksi na Wakatoliki kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 10 Septemba[2].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.