Nenda kwa yaliyomo

Kindi (mnyama)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Myosciurus)
Kindi
Kindi-jua kijivu (Heliosciurus gambianus)
Kindi-jua kijivu (Heliosciurus gambianus)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Rodentia (Wagugunaji)
Nusuoda: Sciuromorpha (Wanyama kama kindi)
Familia: Sciuridae
Muirhead, 1819
Ngazi za chini

Nusufamilia 5; jenasi 8 katika Afrika:

Kindi ni wanyama wadogo wa familia Sciuridae. Spishi nyingine huitwa kidiri au kuchakulo. Wanatokea Amerika, Ulaya, Asia na Afrika na wamewasilishwa katika Australia. Takriban spishi zote huishi mitini, lakini kuchakulo huishi ardhini. Mkia wa kindi una urefu karibu na ule wa mwili, pengine zaidi. Hula mbegu, makokwa, matunda, nyoga, matumba na machipukizi. Wakati ambapo chakula cha kimea ni adimu, kindi hula chakula cha kinyama pia, k.f. wadudu, mayai, ndege wadogo, makinda ya nyoka na wagugunaji wadogo. Spishi kadhaa za tropiki hula wadudu kushinda chakula cha kimea.

Mwainisho

[hariri | hariri chanzo]
  • Nusufamilia Ratufinae – Kindi majitu (jenasi 1, spishi 4)
  • Nusufamilia Sciurillinae – Kindi kibete wa Amerika (spishi 1)
  • Nusufamilia Sciurinae
    • Kabila Sciurini – Kindi wa Amerika, Ulaya na Asia (jenasi 5, mnamo spishi 38)
    • Kabila Pteromyini – Kindi warukaji wa Asia (jenasi 15, mnamo spishi 45)
  • Nusufamilia Callosciurinae
    • Kabila Callosciurini – Kindi wazuri wa Asia (13 genera, nearly 60 species)
    • Kabila Funambulini – Kindi milia wa Asia (jenasi 1, spishi 5)
  • Nusufamilia XerinaeKuchakulo, kindi wa Afrika na vidiri
    • Kabila Xerini – Kuchakulo wa Afrika (jenasi 3, spishi 6)
    • Kabila Protoxerini – Kindi na vidiri (jenasi 6, mnamo spishi 50)
    • Kabila Marmotini – Kuchakulo wa Ulaya, Asia na Amerika (jenasi 6, mnamo spishi 90)

Spishi za Afrika

[hariri | hariri chanzo]

Spishi za kabla ya historia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kindi (mnyama) kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.