Kidiri (mnyama)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Paraxerus)
Kidiri
Kidiri kijivu (Paraxerus cepapi)
Kidiri kijivu (Paraxerus cepapi)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Rodentia (Wagugunaji)
Nusuoda: Sciuromorpha (Wanyama kama kindi)
Familia: Sciuridae (Wanyama walio na mnasaba na kindi)
Muirhead, 1819
Nusufamilia: Xerinae (Wanyama wanaofanana na kindi)
Osborn, 1910
Kabila: Protoxerini (Wanyama wanaofanana sana na kindi)
Jenasi: Paraxerus
Forsyth Major, 1893
Ngazi za chini

Spishi 11:

Kidiri ni wanyama wadogo wa jenasi Paraxerus katika kabila Protoxerini la familia Sciuridae ambao wanafanana sana na kindi. Tofauti na hawa, ambao hukaa mitini takriban saa zote, kidiri hupitisha muda mrefu ardhini lakini hulala katika tundu mtini. Wanatokea misitu mikavu na minyevu ya Afrika. Hula mbegu, makokwa, matunda, matumba, machipukizi na wadudu.

Spishi[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]