Kindi-jua
Mandhari
(Elekezwa kutoka Heliosciurus)
Kindi-jua | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kindi-jua kijivu (Heliosciurus gambianus)
| ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||
Spishi 6:
|
Kindi-jua ni wanyama wadogo wa jenasi Heliosciurus katika kabila Protoxerini la familia Sciuridae. Mkia yao una miviringo myeusi na kahawia au kijivu. Kama kindi wote spishi hizi hupitisha takribani saa zote mitini na huteremka kwa nadra ardhini. Hupatikana mara nyingi wakipumzika juani, sababu ya jina lao. Wanatokea misitu ya Afrika ya Magharibi, ya Kati na ya Mashariki kutoka Senegali mpaka Eritrea na Zimbabwe. Hula mbegu, makokwa, matunda, matumba, machipukizi, wadudu, mayai na mijusi, ndege na wanyama wadogo.
Spishi
[hariri | hariri chanzo]- Heliosciurus gambianus, Kindi-jua Kijivu (Gambian Sun Squirrel)
- Heliosciurus mutabilis, Kindi-jua Kusi (Mutable Sun Squirrel)
- Heliosciurus punctatus, Kindi-jua Mdogo (Small Sun Squirrel)
- Heliosciurus rufobrachium, Kindi-jua Miguu-myekundu (Red-legged Sun Squirrel)
- Heliosciurus ruwenzorii, Kindi-jua wa Ruwenzori (Ruwenzori Sun Squirrel)
- Heliosciurus undulatus, Kindi-jua Mashariki (Zanj Sun Squirrel)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Kindi-jua mdogo
-
Kindi-jua miguu-myekundu
-
Kindi-jua wa Ruwenzori