Nenda kwa yaliyomo

Msumenonyororo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Msumenomashine aina ya Stihl.
Osteotome, iliyotumiwa na madaktari kukata mifupa.
Msumenomashine wa zamani, aina ya Dolmar, ukitumiwa na watu wawili pamoja.

Msumenonyororo (kutoka maneno : msu + meno + nyororo; pia msumenomashine na chensoo kutoka Kiingereza "chainsaw") ni pembejeo muhimu sana kwa watu wanaofanya kazi za kukata au kupogoa miti, kukata matofali na pia kuchonga barafu kama inavyofanyika katika nchi Ufini wakati wa majira ya baridi. Msumenonyororo pia hutumika katika nchi baridi kuogelea, hasa wakati wa majira ya kipupwe. Msumenonyororo huwa kifaa kinachoweza kubebwa kwa urahisi, chenye meno makali yanayoweza kuzunguka huku yakikata na kusaga mbao kuzifanya ziwe ndogo.

Historia

Historia ya msumenonyororo yadhihirisha kwamba kifaa cha kwanza cha namna hiyo kilitengenezwa mwaka 1830 na daktari mmoja wa mifupa Mjerumani kwa jina Bernhard Heine. Hata kama hakikuwa kama msumenonyororo, kifaa hiki kwa jina Oseotome kilikuwa kinafanana kabisa na msumenonyororo tunaojua leo. Kifaa hiki kilitumika haswa kwa kukata mifupa, maana ndiyo iliyokuwa kazi yake daktari Benhard Heine.

Mfano wa awali wa msumenonyororo tunaojua leo ulianzishwa na madaktari wawili wa kutoka nchini Uskoti kwa majina John Aitken na James Jeffray mwishoni mwa karne ya 18.

Muundo

Injini

Msumenonyororo huwa umeundwa kwa kutumia injini (kwa Kiingereza: "engine") inayotumia petroli, au mota ya kielektroni inayotumia nguvu za betri.

Nyororo

Msumenonyororo huzungushwa na nyororo (chain) inayotumia injini au elektroniki ili ianze kazi. Inapozunguka nyororo hii, huweza kuvuta meno ambayo yanasaga mbao, barafu, mfupa au chochote kinachoelekezwa pale.

Msumeno

Msumenonyororo huwa na msumeno wenye meno makali ambayo hunolewa mara kwa mara ili kuyatia makali. Huenda msumeno huu ukavunjika na kwa hivyo inabidi kuubadilisha.

Chuma elekezi

Chuma elekezi (guide bar) ndio humpa mtumiaji mashiko ili aweze kukata. Msumenonyororo mzuri utakuwa na chuma elekezi nzuri isiyoweza kuvunjika kwa haraka.

Vishimo vya mafuta (oil holes)

Injini ya msumenonyororo yahitaji kuwa na mafuta ya kulainisha ili iweze kufanya kazi vizuri. Kifaa hiki basi huwa na vishimo vidogovidogo ambapo mtumiaji huweza kutia mafuta ya kulainisha. Mtumiaji hushauriwa kuwa asingojee hadi wakati mafuta yameyeyuka ili atie mengine. Yafaa awe akiyaweka mara kwa mara.

Kawi ya msumenonyororo

Msumenonyororo ni kati ya vifaa vinavyojulikana kwa Kiingereza kama "power tools" na hutumia kawi ya umeme, hewa iliyozuiliwa, upepo, maji yanayotiririka kama yale ya mto, injini za mvuke pamoja na kawi inayopatikana baada ya kuchoma fuwele.

Aina

Kuna aina tofauti za msumenonyororo kama vile Husqvarna, Makita, Dewalt, Oregon, Echo na nyinginezo.

Ukarabati

Msumenonyororo wafaa kukarabatiwa mara kwa mara maana nyororo yaweza ikakatika, injini ikafeli au hata chuma elekezi ikavunjika. Ukarabati wa msumenonyororo ni pamoja na:

  1. Kuusafisha baada ya matumizi
  2. Kulainisha injini mara kwa mara
  3. Kubadilisha betri au petroli ikiisha
  4. Kunoa meno ya msumenonyororo.

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.