Nenda kwa yaliyomo

Victoria Falls

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mosi-oa-Tunya)
Maporomoko ya Viktoria.
Mosi oa Tunya.

Victoria Falls au Maporomoko ya Viktoria (Mosi-oa-Tunya) ni maporomoko ya mto Zambezi mpakani mwa Zambia na Zimbabwe.

Mto Zambezi wenye upana wa mita 1170 unafika penye ngazi ya mwamba na maji yote yaanguka kimo cha takriban mita 110 yanapoendelea katika mfereji wa mwamba wenye upana wa m 120 pekee. Maporomoko hayo ni makubwa kabisa katika Afrika.

Wenyeji wameyaita "mosi oa tunya" (moshi wa ngurumo) kwa sababu manyunyizo wa maji yaonekana juu ya maporomoko kama wingu la moshi na sauti ya anguko la maji yasikika mbali.[1]

Jina la Victoria Falls limetokana na David Livingstone aliyekuwa Mzungu wa kwanza kuona maajabu hayo mwaka 1856. Alichagua jina hilo kwa heshima ya malkia Viktoria wa Uingereza.[1]

Tangu mwaka 1989 Victoria Falls imepokewa katika orodha ya "urithi wa dunia" wa UNESCO.

Kuna miji miwili inayopokea wageni wanaopenda kutembelea maporomoko hayo. Upande wa Zambia kuna mji wa Livingstone na upande wa Zimbabwe ni mji wa Victoria Falls.

Victoria Falls imewahi kuwa kitovu hasa, lakini tangu kuporomoka kwa uchumi wa Zimbabwe chini ya serikali ya Mugabe idadi kubwa ya watalii hufika upande wa Zambia.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. 1.0 1.1 "Victoria Falls". World Digital Library. 1890–1925. Iliwekwa mnamo 2013-06-01.{{cite web}}: CS1 maint: date format (link)
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Victoria Falls kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.