Maporomoko ya Iguazu
Mandhari
Maporomoko ya Iguazu ni idadi ya maporomoko ya maji kwenye mto Iguazu ambayo yanapatikana kwenye mpaka wa Argentina na Brazil. Kuna maporomoko 275 ya maji kandokando, mengine yenye kimo cha mita 82. Maporomoko hayo yanagawa mto Iguazu katika sehemu mbili, yaani Iguaco ya juu na Iguaco ya chini.
Maporomoko ya Iguazu ni kati ya maporomoko makubwa na mashuhuri zaidi duniani: yanapokea maelfu ya watalii kila mwaka.
Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika Kusini bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Maporomoko ya Iguazu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |