Victoria Falls (mji)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Maporomoko ya Victoria Falls pamoja na daraja kati ya Zimbabwe na Zambia

Victoria Falls ni mji mdogo wa mkoa wa Matabeleland North nchini Zimbabwe mwenye wakazi 16,800 (1992). Uko kando la mto Zambezi mahali unapotelemka kwenye maporomoko ya Victoria Falls.

"Vic Falls" jinsi inavyoitwa kwa kifupi ina mawasiliano kwa barabara na reli kwenda Hwangwe (109 km) na Bulawayo (440 km) upande wa kusini-mashariki. Mji wa karibu ni Livingstone katika Zambia ng'ambo ya mto. Daraja launganisha miji yote miwili.

Mji ulianzishwa mwaka 1901 ukastawi kama kituo cha reli karibu na maporomoko. Ulikuwa kitovu cha utalii kwenye maporomoko. Tangu mwaka 2000 utalii umerudi nyuma kutokana na matatizo ya kiuchumi ya Zimbabwe.