Nenda kwa yaliyomo

Mlonge

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Moringa oleifera)
Mlonge
(Moringa oleifera)
Milonge
Milonge
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Eudicots (Mimea ambayo mche wao una majani mawili)
(bila tabaka): Rosids (Mimea kama mwaridi)
Oda: Brassicales (Mimea kama kabichi)
Familia: Moringaceae (Mimea iliyo na mnasaba na mlonge)
Jenasi: Moringa
Spishi: M. oleifera
Lam., 1785

Mlonge, mlongo, mronge, mrongo, mkimbo au mzunze (Moringa oleifera) ni mti wa jenasi pekee, Moringa, ya familia Moringaceae. Asili ya mti huu ni Uhindi lakini siku hizi hupandwa mahali pengi pa kanda za tropiki na nusutropiki. Hutumika kwa kulisha mifugo, chakula cha watu, kuboresha mashamba, kusafisha maji ya kunywa na mitishamba. Majani yake ni chakula bora (mboga chungu), lakini maganda mabichi, maua, mbegu, mafuta ya mbegu na mizizi hulika pia.

Mti wa mlonge pia umegundulika kuwa ndio mti wenye maajabu zaidi duniani hasa baada ya kufanyiwa utafiti na wanasayansi wa Uingereza. Mti huu una uwezo wa kutibu magonjwa zaidi ya 100 kama vile vidonda vya tumbo, malaria, homa ya matumbo, maambukizo ya mfumo wa mkojo na magonjwa mengine. Mti huu pia umeonekana kuwa na protini nyingi kuliko inayopatikana katika nyama, maziwa, samaki pamoja na maharagwe. Pia mti huu una virutubisho vya Omega-3 ambavyo havipatikani katika maziwa na nyama hivyo kuwa ndio mti wa ajabu zaidi duniani.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mlonge kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.