Nenda kwa yaliyomo

Muhammad Ali

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mohammed Ali)

Kwa watu wengine wenye jina hili tazama Muhammad Ali (maana)

Muhammad Ali

Takwimu
Jina Muhammad Ali
Jina la kuzaliwa Cassius Marcellus Clay Jr.
Jina la utani The Greatest, The Champ,
The Louisville Lip
Urefu 1.91 m (6 ft 3 in)
Kufikia 2 M
Aina ya michezo Mchezo wa ngumi
Mgawanyiko wa uzito Uzito mkubwa
Utaifa Marekani
Tarehe ya kuzaliwa 17 Januari 1942 (1942-01-17) (umri 82)
Mahala pa kuzaliwa Louisville, Kentucky, U.S.
Msimamo Orthodox
Rekodi ya ndondi
Jumla ya mapigano 61
Ameshinda 56
Alizoshinda kwa kuangusha 37
Alizopteza 5
Sare 0
Pambano asiloshiriki 0

Muhammad Ali (jina la awali: Cassius Marcellus Clay Jr.; mnamo 17 Januari 1942 - 3 Juni 2016) alikuwa mwanamasumbwi kutoka nchini Marekani. Alipata kuwa bingwa wa uzito wa juu mara tatu. Katika mchezo wa ngumi anatazamwa kama mmoja wa wanamasumbwi bora wa uzito wa juu wa muda wote.

Wakati akiwa mwanamasumbwi wa ndondi za ridhaa, alishinda medali ya dhahabu ya uzito wa chini kwenye mashindano ya Olimpiki ya mwaka wa 1960 yaliyofanyika mjini Roma, Italia.

Baada ya kuwa mwanamasumbwi wa kulipwa, alikwenda kuwa mwanandondi wa kwanza kushinda mara tatu daraja la lineal. Mnamo mwaka wa 1999, Ali alipewa taji la "Mwanamichezo wa Karne" na Sports Illustrated na "Mwanamichezo Mashuhuri wa Karne" na BBC.[1]

Anafahamika sana kwa staili ya upiganaji wake, ambapo aliielezea staili yake kuwa ni "napaa kama kipepeo, nauma kama nyuki".[2]

Awali alijulikana kama Cassius Clay, lakini alibadilisha jina lake baada ya kujiunga na jumuia ya Kiislamu ya Nation of Islam mnamo mwaka wa 1964. Baadaye akabadilisha dini na kuwa Mwislamu kunako mwaka wa 1975.

Mnamo mwaka wa 1967, Ali alikataa kuwekwa katika orodha ya majeshi ya Marekani kutokana na imani ya kidini na kupinga vita dhidi ya Vietnam. Alikamatwa na kupatikana na hatia juu ya rasimu ya ukwepaji mashtaka, wakamvua taji lake la uanamasumbwi, na leseni yake ya uanamasumbwi ikazuiliwa. Hakufungwa, lakini hakupambana kwa takriban miaka minne mpaka hapo rufaa yake ilipofanyiwa kazi na Mahakama Kuu ya Marekani, ambapo akaja kushinda.

  • Hauser, Thomas (2004). Muhammad Ali: His Life and Times. Robson Books. ISBN 1861057385. OCLC 56645513.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Muhammad Ali kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.