Mlalo
Mlalo ni kata ya Wilaya ya Lushoto katika Mkoa wa Tanga, Tanzania. Msimbo wa posta ni 21721.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 7,589 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ina wakazi wapatao 8,143 waishio humo.
Kuna vijiji vya Mlalo, Msale, Kibandai, Ngazi, Mgwashi, Baghai na Bungoi.
Mlalo iko kwenye kimo cha mita 1450 juu ya usawa wa bahari magharibi mwa milima ya Usambara. Ni eneo lililokaliwa na Washambaa kabla ya enzi ya ukoloni[2].
Misheni ya Kilutheri
[hariri | hariri chanzo]Mnamo mwaka 1889 Wajerumani Baumann na Hans Meyer walikuta huko makao makuu ya mwene Sikinyassi[3] aliyetawala maeneo ya Usambara kaskazini.[4]
Kazi ya kanisa la Kilutheri kwenye milima ya Usambara ilianzia Mlalo. Mnamo mwaka 1891 wamisionari Walutheri Ernst Johanssen na Paul Wohlrab kutoka shirika la misioni Bethel katika Ujerumani walifika huko. Walikataa kusindikizwa na polisi ya kikoloni kwa sababu hawakutaka kuanzisha misioni yao kwa nguvu ya silaha[5]. Walipata kibali cha mwene Sikinyasi wakaanzisha kituo cha "Hohenfriedeberg"[6] (Kijerumani kwa mlima mrefu wa amani). Pamoja na kujenga kanisa, walianzisha pia kituo cha kuwahudumia wenye ukoma.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.nbs.go.tz
- ↑ [http://web.archive.org/20210613165228/http://www.ub.bildarchiv-dkg.uni-frankfurt.de/Bildprojekt/Lexikon/php/suche_db.php?suchname=Mlalo Ilihifadhiwa 13 Juni 2021 kwenye Wayback Machine. Mlalo katika Kamusi ya Koloni za Kijerumani]
- ↑ Sikinyassi au Si -Kiniass ni namna jinsi Wajerumani waliandika jina la mwene; wasomaji wenyeji wanaweza kusaidia hapa kama ni jina lilelile la mwene mashuhuri Kinyashi
- ↑ Usambara und seine Nachbargebiete. Allgemeine Darstellung des nordöstlichen Deutsch - Ostafrika und seiner Bewohner Oscar Baumann, Berlin 1891, uk. 179
- ↑ Usambara ein neues Missionsgebiet, tovuti ya Misioni ya Bethel, iliangaliwa Februari 2017
- ↑ [http://web.archive.org/20210613173102/http://www.ub.bildarchiv-dkg.uni-frankfurt.de/Bildprojekt/Lexikon/php/suche_db.php?suchname=Hohenfriedeberg Ilihifadhiwa 13 Juni 2021 kwenye Wayback Machine. Kamusi ya Koloni za Kijerumani], makala Hohenfriedeberg
Kata za Wilaya ya Lushoto - Mkoa wa Tanga - Tanzania | ||
---|---|---|
Dule "M" | Gare | Hemtoye | Kilole | Kwai | Kwekanga | Kwemashai | Kwemshasha | Lukozi | Lunguza | Lushoto | Magamba | Makanya | Malibwi | Malindi | Manolo | Mbaramo | Mbaru | Mbwei | Migambo | Mlalo | Mlola | Mnazi | Mng'aro | Mtae | Mwangoi | Ngulwi | Ngwelo | Rangwi | Shagayu | Shume | Sunga | Ubiri |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tanga bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mlalo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |