Mlalo (Lushoto)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Mlalo ni jina la kata ya Wilaya ya Lushoto katika Mkoa wa Tanga , Tanzania. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ina wakazi wapatao 8,143 [1] waishio humo. Msimbo wa posta ni 21721. Kuna vijiji vya Mlalo, Msale, Kibandai, Ngazi, Mgwashi, Baghai na Bungoi.

Mlalo iko kwenye kimo cha mita 1450 katika magharibi ya milima ya Usambara. Ni eneo lililokaliwa na Washambaa kabla ya enzi ya kikoloni[2].

Misioni ya Kiluteri[hariri | hariri chanzo]

Mnamo mwaka 1889 Wajerumani Baumann na Hans Meyer walikuta hapa makao makuu ya mwene Sikinyassi[3] aliyetawala maeneo ya Usambara kaskazini.[4] Kazi ya kanisa la Kiluteri kwenye milima ya Usambara ilianza hapa Mlalo. Mnamo mwaka 1891 wamsionari Waluteri Ernst Johanssen na Paul Wohlrab kutoka shirika la misioni Bethel katika Ujerumani walifika hapa. Walikataa kusindikizwa na polisi ya kikoloni kwa sababu hawakutaka kuanzisha misioni yao kwa nguvu ya silaha[5]. Walipata kibali cha mwene Sikinyassi wakaanzisha kituo cha „Hohenfriedeberg“ (jer. kwa mlima mrefu wa amani). Pamoja na kujenga kanisa hapa walianzisha pia kituo cha kuwahudumia wenye ukoma.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Sensa ya 2012, Tanga - Handeni DC[dead link]
  2. Mlalo katika Kamusi ya Koloni za Kijerumani
  3. Sikinyassi au Si -Kiniass ni namna jinsi Wajerumani waliandika jina la mwene; wasomaji wenyeji wanaweza kusaidia hapa kama ni jina lilelile kama jina la mwene mashuhuri Kinyashi
  4. Usambara und seine Nachbargebiete. Allgemeine Darstellung des nordöstlichen Deutsch - Ostafrika und seiner Bewohner Oscar Baumann, Berlin 1891, uk. 179
  5. Usambara ein neues Missionsgebiet, tovuti ya Misioni ya Bethel, iliangaliwa Februari 2017
Flag-map of Tanzania.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tanga bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mlalo (Lushoto) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.
Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Lushoto - Mkoa wa Tanga - Tanzania Flag of Tanzania.svg

Baga | Bumbuli | Dule "B" | Dule "M" | Funta | Gare | Hamtoye | Kilole (Lushoto) | Kwai | Kwekanga | Kwemashai | Kwemshasha | Lukozi | Lunguza | Lushoto | Maheza Ngulu | Makanya | Malibwi | Malindi | Mamba | Manolo | Mayo | Mbaramo | Mbuzii | Mgwashi | Milingano | Mlalo | Mlola | Mnazi | Mng'aro | Mponde | Mtae | Mwangoi | Ngulwi | Ngwelo | Nkongoi | Rangwi | Shume | Soni | Sunga | Tamota | Ubiri | Usambara | Vuga