Nenda kwa yaliyomo

Mkukusu (entandrophragma excelsum)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mkukusu kwenye mlima Kilimanjaro (picha ya A Hemp)

Mikukusu (jina la kisayansi: exandrophragma excelsum) ni kati ya miti mirefu zaidi duniani. Mazingira asilia yapo barani Afrika kwenye maeneo ya kitropiki ya Afrika Mashariki ikitokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda, Burundi, Uganda, Tanzania, Malawi na Zambia.

Miti hii inapatikana kwa hali ya mtawanyiko kwenye misitu ya milimani kwenye kimo cha mita 1000 hadi 2150 juu ya UB.

Kwa kawaida entandrophragma excelsum inapatikana kwa urefu wa mita 45 hadi 60, yenye shina refu lisilonyooka.

Mwaka 2016 mifano mirefu ilipimwa pale Tema, kata ya Mbokomu, kwenye mabonde ya mlima Kilimanjaro, Tanzania iliyofikia hadi mita 81.5[1]. Mti huo ni mti mrefu zaidi unaojulikana Afrika. Umekadiriwa kuwa na umri wa miaka 600 hivi[2].

Mifano 10 mirefu zaidi iliyopimwa ilikuwa na urefu wa mita 59 hadi 81.5 na vipenyo vya mita 1.24 hadi m 2.55[3] [4]

Majina mbadala ya kisayansi

[hariri | hariri chanzo]

Yafuatayo ni majina mbadala ya kisayansi ya Entandrophragma excelsum: [5]

  • Entandrophragma deiningeri Harms
  • Entandrophragma gillardini Ledoux
  • Entandrophragma speciosum Harms
  • Entandrophragma stolzii Harms

Majina mengine

[hariri | hariri chanzo]

Majina ya kawaida ya mti wa Entandrophragma extelsum kwa lugha nyingine ni: [6]

  1. Mti mrefu barani Afrika uko Tanzania, ni kivutio watalii , tovuti ya BBC ya tar. 4 Juni 2017
  2. Mti wenye miaka 600 wapatikana nchini, tovuti ya mwanancho.co.tz ya 3.3. 2017
  3. springer.com / Africa’s highest mountain harbours Africa’s tallest trees, First Online: 17 October 2016, Biodiversity and Conservation: January 2017, Volume 26, Issue 1, pp 103–113. Authors: Andreas Hemp, Reiner Zimmermann, Sabine Remmele, Ulf Pommer, Bernd Berauer, Claudia Hemp, Markus Fischer. DOI: 10.1007/s10531-016-1226-3
  4. newscientist.com / Africa’s tallest tree measuring 81m found on Mount Kilimanjaro, By Agata Blaszczak-Boxe, 24 November 2016
  5. theplantlist.org / Entandrophragma excelsum (Dawe & Sprague) Sprague Ilihifadhiwa 11 Novemba 2019 kwenye Wayback Machine.
  6. worldagroforestry.org / Entandrophragma excelsum

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkukusu (entandrophragma excelsum) kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.