Mikaeli de la Mora

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Miguel De La Mora)
Picha yake halisi.

Mikaeli de la Mora (jina kamili kwa Kihispania Miguel de la Mora y de la Mora; Tecalitlán , Mexico, 19 Juni 1874 - 7 Agosti 1927) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki nchini Meksiko hadi alipouawa bila kesi, kwa sababu tu ni padri, wakati wa Vita vya Wakristero[1].

Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri tarehe 22 Novemba 1992 halafu mtakatifu mfiadini tarehe 21 Mei 2000 pamoja na wenzake 24 waliofia dini katika vita hivyo[2]:

Sikukuu yao inaadhimishwa kila tarehe 21 Mei ila ya kwake mwenyewe ni tarehe ya kifodini chake[3].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.