Nenda kwa yaliyomo

Kunguni-makasia kibete

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Micronectidae)
Kunguni-makasia kibete
Micronecta scholtzi
Micronecta scholtzi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye mwili wa pingili na miguu ya kuunga wasio na ugwe wa mgongo kama wadudu, nge, buibui)
Nusufaila: Hexapoda (Arithropodi wenye miguu sita)
(bila tabaka): Dicondylia (Wadudu walio na mandibula zenye condyle mbili)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Nusungeli: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda ya juu: Paraneoptera
Oda: Hemiptera
Haeckel, 1896
Nusuoda: Heteroptera
Oda ya chini: Nepomorpha
Familia ya juu: Corixoidea
Familia: Micronectidae
Jaczewski, 1924
Ngazi za chini

Nusufamilia 2, jenasi 7, 1 katika Afrika ya Mashariki:

Kunguni-makasia vibete ni wadudu wadogo sana wa maji wa familia Micronectidae katika oda ya chini Nepomorpha ya oda Hemiptera wanaoogelea chini ya uso wa maji kwa msaada wa miguu yao ya nyuma inayofanana na makasia. Kwa hivyo wanafanana na kunguni-makasia wadogo. Wanafanana pia na waogeleaji-juuchini vibete kwa ukubwa, lakini hao huogelea juu chini kwa wazi. Kunguni-makasia vibete wanatokea duniani kote isipokuwa Antakitiki.

Kunguni-makasia vibete wana urefu wa mm 1-5. Wanaonekana takriban sawa na kunguni-makasia, lakini ni wafupi ikilinganishwa na upana wao na hawana mistari iliyopitilia upande hadi upande mgongoni; spishi fulani zina mabaka. Pia wana miguu mifupi ya mbele na miguu mirefu ya kati na ya nyuma, ile ya mwisho ikitumika kwa kuogelea. Inaonekana kama wadudu wengine wa spishi moja hawana mabawa na wengine wanayo.

Biolojia

[hariri | hariri chanzo]

Wadudu hawa huogelea chini ya uso wa maji, mara nyingi katika makundi makubwa. Kidogo kinajulikana kuhusu upendeleo wao wa chakula, lakini ushahidi unaopatikana unaonyesha lishe mbalimbali na tofauti kati ya spishi. Kwa idadi ya spishi, chakula kinajulikana kuwepo kwa viani, protozoa, bakteria, minyoo wadogo na viluwiluwi[1].

Kunguni-makasia vibete wanatokea kwenye maji yasiyo na kina kirefu, ikiwezekana mahali ambapo samaki hawapo, kama madimbwi madogo na kingo za maziwa. Baadhi ya spishi wanajulikana kufyonza oksijeni iliyoyeyushwa na kwa hivyo wanapendelea kuishi katika maji safi yenye kiwango cha juu cha oksijeni. Walakini, spishi chache zinaweza kuishi katika maji machafu yenye kiwango cha chini cha oksijeni na yamkini hupumua hewa angalau kwa sehemu. Kwa hivyo, wadudu hawa wanaweza kutumika kama viashirio vya ubora wa maji[1].

Kidogo pia kinajulikana kuhusu tabia ya kupandana na mzunguko wa maisha. Inachukuliwa kuwa hizi ni sawa na kunguni-makasia. Walakini, tofauti moja ni kwamba madume hutoa sauti kwa kusugua uume wao kwenye mwinuko wa pingili 8 ya fumbatio, huku kunguni-makasia wakisugua miguu yao ya mbele dhidi ya kichwa chao[1].

Spishi kadhaa za Afrika

[hariri | hariri chanzo]
  • Micronecta abyssinica
  • Micronecta algirica
  • Micronecta bleekiana
  • Micronecta browni
  • Micronecta butleriana
  • Micronecta citharistia
  • Micronecta dimidiata
  • Micronecta dorothea
  • Micronecta druryana
  • Micronecta gorogaiqua
  • Micronecta mauritania
  • Micronecta mutile
  • Micronecta peralita
  • Micronecta scholtzi
  • Micronecta scutellaris
  • Micronecta uvarovi
  • Micronecta winifreda
  • Micronecta youngiana