Nenda kwa yaliyomo

Mitrofani Chi Sung

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Metrophanes, Chi Sung)
Picha yake halisi ya mwaka 1882 alipokuwa Tokyo, Japani.
Picha takatifu ya Wafiadini Waorthodoksi wa China.

Mitrofani Chi Sung (Cháng Yángjí,常楊吉; 10 Desemba 185510 Juni 1900) alikuwa padri wa kwanza wa Kanisa la Kiorthodoksi la China kufia dini ya Ukristo.

Alikuwa amekubali kwa shida kupewa upadrisho huko Tokyo, Japani mwaka 1880, akijiona hana sifa.

Ndiye maarufu zaidi kati ya wafiadini wa China 222 wa Kanisa hilo waliotangazwa watakatifu mwaka 2000[1], wakiwemo watu wa familia yake (mke Tatiana Li na watoto Isaya na Yohane).

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 11 Juni.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]