Metorolojia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Ramani inayoonyesha halijoto wastani ya uso wa bahari. Ramani za aina hii ni tokeo ya miaka mingi ya vipimo na pia msaada muhimu kwa kuelewa utaratibu wa mabadiliko ya halihewa kama kutokea kwa dhoruba au kunyesha au kutonyesha kwa mvua

Metorolojia (Kigir. μετεωρολογία meteorologia kuwa kiing. meteorology) ni sayansi inayoshughulika habari za angahewa, tabianchi na halihewa na hasa fizikia pamoja na kemia husika.

Tabia za angahewa[hariri | hariri chanzo]

Tabia za kimsingi za hali ye hewa ni mwendo wa upepo, halijoto, umawingu, unyevu, kanieneo, kiwango cha mnururisho wa jua, uvukizaji na nyingine. Tangu karne nyingi wataalamu wamejitahidi kupima tabia mbalimbali za halihewa na angahewa kama msaaa wa kuzielewa vizuri zaidi na kujenga msingi kwa utabiri wake.

Vifaa vya metorolojia[hariri | hariri chanzo]

Metorolojia imeanza kutokea kadri wataalamu walianza kuchukua vipimo halisi vya tabia za angahewa na kuvilinganisha. Mweleko huu ulileta kubuniwa kwa vifaa vya upimaji maalumu.

  • vyombo vya kupima kiasi cha usimbishaji hasa mvua vilivyosanifishwa na serikali vinajulikana kutoka Korea mnamo 1441; vilisambazwa kama msaada wa kukadiria kodi za wakulima. Hadi leo kiasi cha mvua kinachonyesha kwa mwezi au mwaka ni kipimo muhimu kwa kupanga shughuli za kilimo.
  • vyombo vya kupima kasi na mwelekeo wa upepo kwa mahali fulani vinajulikana tangu anemomita iliyobuniwa Italia mnamo 1450. Habari hizi ni za kimsingi kwa kuelewa uhusiano kati ya hali ya hewa katima maeneo majirani; ni pia muhimu kwa kupanga kilimo kwa sababu zinatawala sehemu ya uvukizaji na ni habari za lazima kwa mpangilio wa usafiri kwa eropleni na pia meli.
  • Vipimajoto vilivyofanana na vile vya kisasa vilipatikana tangu karne ya 17 na 1724 Daniel Gabriel Fahrenheit alianzsha skeli ya kwanza iliyoruhusu kulinganishwa kwa vipimo vya joto.
  • Higromita ni kifaa cha kupima kiwango cha unyevu katika hewa na chombo hiki kilibuniwa 1783 na Mfaransa Horace-Bénédict de Saussure.