Nenda kwa yaliyomo

Metodi I wa Konstantinopoli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha takatifu ya ushindi wa imani sahihi. Metodi amechorwa upande wa juu kulia.

Metodi I wa Konstantinopoli (Siracusa, leo nchini Italia, 788 hivi – Konstantinopoli, leo nchini Uturuki, 14 Juni 847) alikuwa mmonaki na mwandishi wa Kikristo wa Dola la Bizanti.

Alifungwa gerezani kwa sababu ya kutetea matumizi ya picha takatifu hata mbele ya Papa Paskali I huko Roma , lakini hatimaye akawa Patriarki wa Konstantinopoli tangu 4 Machi 843 hadi kifo chake akishuhudia ushindi wa imani sahihi[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi na Wakatoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 14 Juni[2].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.