Maria Ana wa Yesu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mchoro wa Francisco Sylverio de Sotomayor (karne ya 18) kuhusu Mariana de Jesús, Azucena de Quito, Heroina Nacional y Virgen Penitente.

Maria Ana wa Yesu (jina kamili la Kihispania ni Mariana de Jesús Paredes y Flores) alizaliwa Quito (Ekwador) tarehe 31 Oktoba 1618 akafariki huko tarehe 26 Mei 1645.

Bikira huyo wa Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu tangu tarehe 4 Juni 1950, alipotangazwa na Papa Pius XII. Kabla yake, Papa Pius IX alikuwa amemtangaza mwenye heri tarehe 20 Novemba 1853.

Ni mtu wa kwanza kutoka Ekwador, na Mfransisko wa kwanza kutoka Amerika Kusini kutangazwa mtakatifu.

Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe 26 Mei.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Christian cross.svg Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Maria Ana wa Yesu kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.