Nenda kwa yaliyomo

Quito

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Jiji la Quito
Nchi Ekuador
Kanisa la Quito
Quito

Quito (tamka: "kito" - Kihisp. "San Francisco de Quito") ni mji mkuu wa Ekuador. Mwaka 2005 ilikuwa na wakazi 1,865,541. Quito ni mji mkubwa wa pili nchini baada ya Guayaquil.

Mji uko 20 km kusini ya mstari wa ikweta katika bonde la milima ya Andes kwenye kimo cha 2850 m juu ya UB.

Kuna kiwanja cha ndega na chuo kikuu pamoja na viwanda.


Quito

Guápulo de Quito

[hariri | hariri chanzo]
TelefériQo

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Quito ilikuwa kati ya miji muhimu ya Dola la Inka kabla ya kufika kwa Wahispania. Wakati wa uvamizi wa Wahispania jenerali Rumiñahui wa jeshi la Inka alichoma mji na kuiharibu kabisa kabla ya Wahispania hawakuiteka.

Quito iliundwa upya na Sebastián de Belalcázar mwaka 1534.

Mwaka 1809 wakati wa ghasia katika sehemu mbalimbali za Amerika Kusini dhidi ya serikali ya mfalme mpya wa Hispania Joseph Bonaparte (mdogo wake Napoleon Bonaparte) kamati ya raia katika Quito ilitangaza uhuru wa eneo lake kutoka Hispania. Utawala wa Hispania ulirudishwa kwa mabavu hadi 1822 wakati Hispania ilishindwa na mapinduzi ya Simon Bolivar na kuundwa kwa jamhuri ya Gran Colombia. Baada ya mwisho wa jamhuri hii sehemu zake ziliachana Quito ikawa mji mkuu wa nchi mpya ya Ekuador.

Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Quito kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: