Nenda kwa yaliyomo

Sebastián de Belalcázar

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sebastián de Belalcázar

Sebastián de Belalcázar alikuwa conquistador (mwanajeshi) Mhispania. Alizaliwa Cordoba (Hispania) mnamo 1479 au 1480.

Mwaka 1507 alihamia Amerika katika koloni mpya za Hispania. Akajiunga na kikosi cha Francisco Hernández de Córdoba mwaka 1524 aliyefanya Nikaragua kuwa koloni ya Hispana akawa meye ya kwanza wa mji wa Leon (Nikaragua).

Kupitia Honduras alisafiri kwenda Peru alipojiunga na jeshi la Francisco Pizarro mwaka 1532.

1534 alishambulia mji wa Quito katika Ekuador lakini mji ukachomwa na jenerali Rumiñahui wa jeshi la Inka. Belalcazar aliunda mji upya mwaka uleule kwa jina la "San Francisco de Quito".

1535 alielekea kaskazini katika Kolombia ya leo akitafuta dhahabu. Akaunda miji ya Pasto, Santiago de Cali na Popayan katika miaka 1536 na 1537.

Picha ya Belalcázar kwenye pesa ya Ekuador

Katika miaka iliyofuata aliingia katika nyanda za juu za Kolombia akapewa cheo cha gavana wa Popayan na Kaisari Karolo V mwaka 1540. Akaingia katika mapigano na magavana majirani juu ya maeneo akamwua jirani mmoja akapata hukumu ya mauti.

Alipopanga safari ya Hispania kwa kusudi la kujitetea alikufa mwaka 1551 mjini Cartagena (Kolombia).

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]