Nenda kwa yaliyomo

Conquistador

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Hernando Cortes conquistador wa Meksiko

Conquistador (tamka: kon-kis-ta-dor; uzito kwa silabi ya mwisho) ni neno la Kihispania ya kutaja jumla la wanajeshi, wapelelezi, mabaharia na wengine kutoka Hispania na Ureno waliovamia nchi za Amerika ya Kilatini na Pasifiki na kuzifanya kuwa koloni za Kihispania na za Kireno.

Harakati ya uvamizi na utekaji wa Amerika ya Kilatini huitwa kwa Kihispania kwa neno "Conquista" (=utekaji).

Katika karne baada ya Kristoforo Kolumbus watekaji walikuwa watu waliotafuta utajiri na heri katika "dunia mpya" ya Amerika. Mara nyingi walikuwa wanajeshi wa kustaafu waliokosa nafasi katika maisha ya kawaida Hispania. Walifanya misafara yao kwa gharama zao bila msaada wa serikali ya Hispania au Ureno.

Isipokuwa walitangulia kujipatia kibali cha kifalme. Conquistador alipata kibali cha kuvamia eneo fulani kwa jina la mfalme wa Hispania lililoelezwa katika kibali ingawa mara nyingi maeneo hayajulikana bado. Alitakiwa kujenga vituo na miji na kuwapeleka wenyeji wakubali imani ya kikristo yaani ya kanisa katoliki. Kibali kilieleza pia masharti yote kuhusu forodha la bishaa zitakazoingia au kutoka katika koloni mpya. Sehemu ya tano ya mapato yote (= 20%) ya koloni ilitakiwa kulipwa kwa serikali.

Conquistador mwenye kibali alipata haki ya kumteua gavana na wasimamizi wa koloni mpya.

Maconquistador wengine waliomfuata mwenye kibali mara nyingi hawakuwa wanajeshi wa kawaida kwa sababu wengi walikosa pesa ya kuwalipa. Wengine waliingia kama washiriki katika biashara ya koloni walioahidiwa asilimia fulani ya faida.

Kuanzia mwaka 1600 nafasi ya Maconquistador ilipungua na kuisha kwa sababu serikali ya Hispania ilifaulu kueneza utawala wake kwa utaratibu wa falme dogo.

Maconquistador walitafuta utajiri kwa kila namna na mara nyingi waliwatendea wenyeji kwa unyama mkuu. Silaha zao pamoja na farasi ziliwawezesha kushinda jeshi kubwa za wenyeji ambao kwa ujumla walikuwa na silaha za mawe tu na ambao hawakuona farasi wala mtu juu ya farasi. Waliweza kuharibu miliki kubwa za Maazteki na Mainka.

Balaa mbaya zaidi kushinda unyama wote yalikuwa magonjwa kutoka Ulaya yaliyoua mamilioni wa Maindio waliokosa kinga dhidi ya viini vilivyofika Amerika mara ya kwanza.

Baada ya kufaulu maconquistador walijaribu mara nyingi kudanganya serikali au wenzao hivyo mara nyingi kuunda kwa koloni mpya kulimalizika mbele ya mahakama.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Conquistador kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: