Francisco Pizarro

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Francisco Pizarro mnamo 1540

Francisco Pizarro alikuwa conquistador (mwanajeshi) Mhispania aliyevamia Peru na kuharibu Dola la Inka mwaka 1533.

Pizarro alizaliwa 1471 (au 1478) mjini Trujillo (Hispania). Mwaka 1509 aliondoka Hispania kwenda Amerika katika koloni mpya za Hispania.

Pizarro hakujua kuandika akachora alama mbili tu na karani akaongeza maandishi ya jina.

Miaka ya Upelelezi katika Amerika Kusini[hariri | hariri chanzo]

Alipokaa miaka kadhaa katika Panama Pizarro alisikia habari za nchi tajiri katika kusini iliyoitwa "Piru". Alifanya safari tatu akifuata mwambao wa Kolombia na Ekuador akafika katika mji wa Tumbes uliokuwa tayari sehemu ya Dola la Inka alipopokelewa vizuri.

Pizarro akarudi Hispania akajipatika kibali cha Kaisari Karolo V ya kuwa gavana wa Peru akifaulu kuvamia na kuteka nchi ile isiyojulikana hadi wakati ule kama angeweza kufaulu kwa gharama zake mwenyewe.

Uvamizi wa Peru[hariri | hariri chanzo]

1531 alitoka Panama kwa jahazi 3 na watu 207. Mwezi wa Agosti 1532 aliunda Piura kama mji wa kwanza wa Kihispania nchini Peru. Katika Septemba aliongoza jeshi lake kuelekea nyanda za juu katika milima ya Andes ambako alisikia angekuta mji mkuu wa Inka.

Inka Atahualpa akamatwa mjini Cajamarca tar. 16 Novemba 1532

Inka Atahualpa anakamtawa[hariri | hariri chanzo]

Tar. 15 Novemba 1532 alifika na jeshi lake la ndogo la watu 180, mzinga mmoja na farasi 27 katika mji wa Cajamarca iliyoko 1000 km kabla ya Cuzco mji mkuu wa Inka. Alikutana na Inka Atahualpa mwenyewe aliyemsubiri na jeshi la askari 20,000 hadi 30,000. Wahispania walifaulu kumwandalia Inka tego kwa kumkaribisha kwa mkutano walipomkamata na kuua maelfu wa walinzi wake waliokutana mara ya kwanza na bunduki, silaha za chuma na wanajeshi juu ya farasi. Jeshi kuu la Inka lilisubiri tu bila kushambulia kwa sababu viongozi waliogopa kumhatarisha Inka mweyewe. Atahualpa alikaa miezi 9 kama mfungwa wa Wahispania.

Pizarro alimwambia Inka Atahualpa ya kwamba atamwachisha huru akijaza chumba kikubwa kwa dhahabu. Inka aliwaamuru watumishi wake kukusanya dhahabu na fedha kote nchini iliyopelekwa Cajamarca. Baada ya kupokea dhahabu Wahispania walimnyonga Athahualpa tar. 29 Agosti 1533.

Mtawala wa Peru[hariri | hariri chanzo]

15 Novemba 1533 Pizarro aliingia bila upingamizi katika mji mkuu wa Cuzco kuuchoma moto. Pizarro alimteua Manco Capac II mdogo wake Athahualpa akamfanya Inka mpya lakini kwa jina tu aliyemsaidia kutawala dola kubwa.

1535 Pizarro aliunda mji mpya ya Ciudad de los Reyes (mji wa wafalme) ulioitwa baadaye Lima ukawa mji mkuu mpya wa Peru.

Jeneza la Pizarro katika kanisa kuu la Lima

Mwisho[hariri | hariri chanzo]

1537 ilitokea fitina kati ya wavamizi Wahispania. Pizarro aliamuru kumwua mpinzani wake Almagro mjini Cuzco. 26 Juni 1541 mfuasi wa Almagro akalipiza kisasi kwa kumwua Pizarro mwenyewe katika jumba lake mjini Lima.

Mara nyingi Pizarro hutazamiwa kama mhuni aliyeharibu utamaduni wa juu, kusababisha mateso na vifo vingi na kuvunja ahadi yake kwa Inka Atahualpa kwa sababu ya hamu ya dhahabu tu.

Uhodari wake wa kijeshi wa kushinda jeshi kubwa sana umempatia sifa kama kiongozi wa kijeshi.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]