Victoria Falls

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Maporomoko ya Mosi oa Tunya)
Jump to navigation Jump to search
Maporomoka ya Viktoria
Mosi oa Tunya

Victoria Falls au Maporomoko ya Viktoria (Mosi-oa-Tunya) ni maporomoko ya mto Zambezi mpakani wa Zambia na Zimbabwe.

Mto wa Zambezi mwenye upana wa mita 1170 unafika penye ngazi ya mwamba na maji yote yaanguka kimo cha takriban mita 110 yanapoendelea katika kanali ya mwamba mwenye upana wa 120 m pekee. Maporomoko haya ni makubwa katika Afrika.

Wenyeji wameiita "mosi oa tunya" (moshi wa ngurumo) kwa sababu nyunyiza ya maji yaonekana juu ya maporomoko kama wingu la moshi na sauti ya anguko la maji yasikika mbali.[1]

Jina la Victoria Falls limetokana na David Livingstone aliyekuwa mzungu wa kwanza wa kuona maajabu haya mwaka 1856. Alichagua jina hili kwa heshima ya malkia Viktoria wa Uingereza.[1]

Tangu 1989 Victoria Falls imepokelewa katika orodha la "urithi wa dunia" wa UNESCO.

Utalii[hariri | hariri chanzo]

Kuna miji miwili inayopokea wageni wanaopenda kutembelea maporomoko haya. Upande wa Zambia kuna mji wa Livingstone na upande wa Zimbabwe ni mji wa Victoria Falls.

Victoria Falls iliwahi kuwa kitovu hasa lakini tangu kuporomoka kwa uchumi wa Zimbabwe chini ya serikali ya Mugabe idadi kubwa ya watalii hufika upande wa Zambia.


Tazama pia[hariri | hariri chanzo]


  1. 1.0 1.1 Victoria Falls (1890-1925). Iliwekwa mnamo 2013-06-01.