Majadiliano ya mtumiaji:Abubakari Sixberth

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na n) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

Idd ninga (majadiliano) 22:03, 23 Aprili 2022 (UTC)[jibu]

Google Translate[hariri chanzo]

Asante kwa michango yako, lakini napaswa kudokeza tatizo. Katika makala ulizoanzisha kuhusu Wilson Kinyonga na George Konyonga nimeona dalili kwamba ulitumia Google Translate bila kusafisha vizuri. Mfano: uliandika "Nyota bora wa Wanyika" kama tafsiri ya Wanyika Super Stars; ambayo kwa Kiswahili haina maana kabisa, tena ni kosa kwa sababu majina hayatafsiriwi. Naomba sana uwe mwangilifu, maana wachangiaji wanaomwaga matini kutoka tafsiri ya komyuta wanazuliwa hapa. Kipala (majadiliano) 10:30, 1 Mei 2022 (UTC)[jibu]

Vizuri kusikia kutoka kwako 217.29.135.51 08:29, 2 Mei 2022 (UTC)[jibu]

Interwiki[hariri chanzo]

Tafadhali urudi kwenye makala zako ulizotafsiri juzi na uongeze interwiki. Kipala (majadiliano) 10:42, 22 Mei 2023 (UTC)[jibu]

Taarifa ya kukuzuia!

Ndugu, imenibidi kukuzuia kwa sababu zinazotajwa chini. Wakati unapokuwa umezuiwa huwezi kuhariri isipokuwa penye huu ukurasa wako wa majadiliano. Unaweza kunijibu kwa kutumia “Email this user”.

Sababu ni kuwa umeingiza matini iliyopatikana kwa njia ya tafsiri ya kompyuta ikiwa na kasoro nzito ya lugha. Umearifiwa kwamba ni marufuku kumwaga matokeo ya google translate katika makala zetu. Wachangiaji wanaopuuza utaratibu huu wanasababisha hasara kubwa kwa Wikipedia yetu na kuwapa wengine kazi kubwa mno ya kusafisha makosa yao.

Bila shaka una nia nzuri kuchangia katika Wikipedia. Tutafurahi kushirikiana nawe lakini ni lazima ufuate utaratibu. Kazi yetu kama wakabidhi ni kulinda mradi huu.

Ukiwa tayari kufuata utaratibu pamoja na kupitia upya matini ulizozileta tayari, naomba uwasiliane nami kwa kufungua ukurasa wangu (bofya jina langu chini) na kuniandikia baruapepe kwa kubofya “Email this user” upande wa kushoto. Hapo nitaweza kukuruhusu tena. Hapo lazima uwezeshe njia kwa kufuata maelezo katika Wikipedia:Email.

Nimeona umetumia tafsiri ya kompyuta bila masahihisho ya kutosha; mifano Faiza Darkhani, Nina Amenta, Malawi Girl Guides Association. Kipala (majadiliano) 20:12, 22 Mei 2023 (UTC)[jibu]

Marekebisho ya Makala ya Faiza Darkhani.[hariri chanzo]

Faiza Darkhani (alizaliwa 1992) ni mwalimu, mwanamazingira na mwanaharakati wa haki za wanawake nchini Afghanistan.[1] Mnamo mwaka 2021, alitajwa katika orodha ya wanawake 100 wa BBC inayojumuisha majina ya wanawake wenye msukumo na ushawishi mkubwa duniani.[2] Darkhani ni miongoni mwa wasomi wachache waliopata elimu ya sayansi ya tabianchi huko Afghanistan.[2] Pia alikuwa mkurugenzi kwenye Shirika la taifa la Kulinda Mazingira katika jimbo la Badakhshan, Afghanistan.[1]

Alisoma chuo kikuu cha Badakhshan pamoja na chuo kikuu cha Putra Malaysia na kupata shahada ya uzamili ya sanyansi katika usanifu wa mazingira.[1] Utafiti wake unahusisha usimamizi endelevu wa mandhari mijini pamoja na usalama wa chakula.[3]

Marejeo

  1. 1.0 1.1 1.2 "BBC 100 Women 2021: Who is on the list this year?", BBC News, 2021-12-07. (en-GB) 
  2. 2.0 2.1 "50 Afghans among BBC’s 100 influential women of 2021". The Frontier Post (kwa en-US). 2021-12-08. Iliwekwa mnamo 2022-04-24. 
  3. Bohn, Katrin; Viljoen, André. "The vision of productive urban landscapes is horizontal and vertical". Productive Urban Landscapes. University of Brighton, UK. Iliwekwa mnamo 2022-04-23. 

Abubakari Sixberth (majadiliano) 08:57, 11 Juni 2023 (UTC)[jibu]