Wilson Kinyonga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wilson Peter Kinyonga (1947Agosti, 1995) alikuwa mwanamuziki mashuhuri nchini Kenya. Wilson Kinyonga kazaliwa nchini Tanzania, Yeye na kaka yake aitwae George Kinyonga ndiyo waanzilishi wa bendi ya rumba Simba Wanyika ambaye baadaye ikazaa Les Wanyika, Nyota bora wa Wanyika na chipukizi wengine. Simba Wanyika iliposambaratika, Les Wanyika ikawa maarufu zaidi. Kifo cha George Peter Kinyonga mnamo Agosti 1995 ilitumika kama msumari wa mwisho wa jeneza kwa Simba Wanyika. Majaribio ya baadaye ya wanachama wa zamani kuunga tena bendi hayakufanikiwa.[1]

Wilson na George Kinyonga walianza muziki katika mji wao wa nyumbani Tanga nchini Tanzania, ambapo ndipo walipojiunga kwenye bendi ya Jamhuri Jazz mwaka 1966. Wao walihamia Arusha mwaka 1970 na wakaanzisha bendi ya Arusha Jazz na kaka yao mwingine, William Kinyonga. Mwaka 1970 walihamia nchini Kenya na kuanzisha Simba Wanyika, ambayo ikaja kuwa moja kati ya bendi mashuhuri kwenye historia ya muziki wa Afrika ya Mashariki.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

https://www.bbc.co.uk/radio1/johnpeel/sessions/1990s/1990/Jul24simbawanyika/

https://web.archive.org/web/20060502153442/http://www.afropop.org/explore/band_info/ID/9/Simba%20Wanyika/

  1. "Wikiwand - Wilson Kinyonga". Wikiwand. Iliwekwa mnamo 2023-02-26.