Msaada:Interwiki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Bofya hapa kuona picha vizuri zaidi

Interwiki ni orodha ya viungo vya mada fulani na makala za kufanana katika wikipedia za lugha nyingine.

Katika ukurasa unaosoma sasa hivi orodha ipo upande wa kushoto nje ya makala chini ya "Lugha zingine". Hapa utaona Deutsch, English, فارسی , Français na kadhalika. Zote ni rangi ya buluu maana ni viungo kwenda kurasa za "Mwongozo wa wikipedia" (Help:Interlanguage links) kwa lugha hizi.

Ukianzisha makala mpya na kuihifadhi utaona bado hakuna majina ya lugha kwa rangi ya buluu.

  • Angalia kwenye dirisha la PC chini kabisa upande wa kushoto.
  • Utaona "Lugha" na chini yake "Add links".
  • Bofya "Add links"
  • Utaona sanduku "Link with page".
  • Ingiza hapa "enwiki" (kwa kawaida, unaweza kuteua pia lugha nyingine..), thibitisha
  • Kwenye sehemu ya "page" andika jina la makala (au la makala uliyotafsiri), thibitisha yote, na tena.

Sasa utaona orodha ya lugha zenye viungo kwenda makala za lugha nyingine. Ni msaada mkubwa kama msomaji anataka kusoma maelezo zaidi kwa Kiingereza na kadhalika. Ni msaada pia kwa wahariri wanaosoma lugha hizo wakitafuta habari za nyongeza.

Jaribu ulichojifunza katika sanduku la mchanga


Soma zaidi katika Wikipedia:Mwongozo_(Viungo_vya_Wikipedia)