Wikipedia:Sanduku la mchanga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Jitahidi sana kuwathamini wengine kwa kuwapenda na kuthamini uwepo wao katika safari yako ya maisha kwa sababu mwanadamu kwa asili yake ni si kisiwa na ndiyo maana anatakiwa aishi na wenzake. Hata wanyama wanaishi pamoja kadiri ya maumbile yao.

Daima kumbuka kujiweka nafasi ya wengine pale unapotaka kuwafanyia kitu chochote kwa kujiuliza kama wewe ungefanyiwa hivyo ungefurahia? Kama unaona wazi kuwa iwapo hicho unachofikiria kutenda kwa wengine usingekifurahia iwapo ungetendewa wewe mwenyewe basi achana nacho.

Siku zote jitahidi kuwatendea wenzako kile ambacho wewe mwenyewe ungependa wengine wakutendee wewe. Mpendwa, kamwe usitarajie kivuli ukiwa unatembea katikati ya jangwa wakati jua kali likiwaka. Namaanisha kuwa kile unachowatendea wenzako nawe siku moja utatendewa na wengine. Kumbe ni vema kuwaheshimu na kuwathamini wenzako kwani kwa kufanya hivyo unajiwekea hazina iliyo bora kabisa.

Kumbuka kuwa sote tunasafiri katika sayari moja na siku moja safari yetu itafikia kikomo yaani tupende tusipende au tukubali tusikubali ukweli ndiyo huo na kamwe hatuwezi kuubadili kwa sababu kubisha ni sawa na kujaribu kuzuia mwanga wa jua kwa kiganja cha mkono wako jambo ambalo kamwe hauwezi kulifanikisha.

Yote hayo yanawezekana iwapo tutajitoa kuwa karibu na Mungu kwa njia ya sala na hapo tutajipatia nguvu ya Kimungu ambayo itatusaidia kuwapenda wenzetu kama Mungu Mwenyewe anavyotupenda.

Hata katika vitabu vya dini {biblia au misaafu} tunaona kuwa Yesu alipokuwa duniani alijitahidi kutenda yale ambayo yalimtukuza Mungu na kuwafurahisha wanadamu .Hivyo basi tunatakiwa kuiga mfano wa Yesu alipo kuwa hapa duniani kwa kujitahidi kuyatenda yele tunayopenda kutendewa kwani "auaye kwa upanga atauawa kwa upanga" na "kipimo uwapimiacho wengine ndicho utakacho pimiwa"

Asanteni sana.