Faiza Darkhani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Faiza Darkhani (alizaliwa 1992) ni mwalimu, mwanamazingira na mwanaharakati wa haki za wanawake nchini Afghanistan.[1] Mnamo mwaka 2021, alitajwa katika orodha ya wanawake 100 ya BBC inayojumuisha majina ya wanawake wenye ushawishi mkubwa duniani.[2] Darkhani ni miongoni mwa wasomi wachache waliopata elimu ya sayansi ya tabianchi huko Afghanistan.[2] Pia alikuwa mkurugenzi kwenye Shirika la Taifa la Kulinda Mazingira katika jimbo la Badakhshan, Afghanistan.[1]

Alisoma chuo kikuu cha Badakhshan pamoja na chuo kikuu cha Putra Malaysia na kupata shahada ya uzamili ya sanyansi katika usanifu wa mazingira.[1] Utafiti wake unahusisha usimamizi endelevu wa mandhari mijini pamoja na usalama wa chakula.[3]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 1.2 "BBC 100 Women 2021: Who is on the list this year?", BBC News, 2021-12-07. (en-GB) 
  2. 2.0 2.1 "50 Afghans among BBC’s 100 influential women of 2021". The Frontier Post (kwa en-US). 2021-12-08. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-02-11. Iliwekwa mnamo 2022-04-24.  More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
  3. Bohn, Katrin; Viljoen, André. "The vision of productive urban landscapes is horizontal and vertical". Productive Urban Landscapes. University of Brighton, UK. Iliwekwa mnamo 2022-04-23.