Nenda kwa yaliyomo

Madeleine Albright

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Madeleine Albright
Madeleine Albright katika Mkutano wa Kimataifa wa Uchumi.
Madeleine Albright katika Mkutano wa Kimataifa wa Uchumi.
Tarehe ya kuzaliwa 15 Mei 1937
Tarehe ya kifo 23 Machi 2022
Kazi mwanamke wa kwanza kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani.


Madeleine Korbel Albright (15 Mei 1937 - 23 Machi 2022) alikuwa mwanamke wa kwanza kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani. Aliteuliwa na Rais Bill Clinton wa Marekani tarehe 5 Desemba 1996, na alikubaliwa bila pingamizi na Bunge la Marekani kwa kura ya 99-0. Aliapishwa tarehe 23 Januari 1997.

Alikosolewa kwa kuunga mkono mashambulio ya NATO dhidi ya Yugoslavia mnamo mwaka 1999. Alihusishwa pia na vifo vya raia wa Irak, hasa watoto[1], kutokana na vikwazo vya kiuchumi vilivyoamuliwa na Baraza la Usalama la UM dhidi ya nchi hiyo[2].

Albright alipozaliwa katika wilaya ya Smíchov mjini Prague, Chekoslovakia, alipewa jina Marie Jana Korbelová. Wakati wa kuzaliwa kwake, nchi hiyo ilikuwa imepata kuwa huru kwa miaka isiyozidi ishirini, kutoka nchi ya Austria baada ya Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia.

Baba yake, Josef Korbel, ambaye alikuwa mwanadiplomasia, alikuwa Mcheki wa Kiyahudi na muungaji mkono wa Wademokrati wa mapema wa Kicheki: Tomáš Garrigue Masaryk na Edvard Beneš. Alikuwa mtoto wa kwanza kutoka kwa bibi yake wa Kiyahudi, Anna (née Spieglová), ambaye baadaye alijifungua msichana mwingine Katherine (mwalimu) na mvulana John (mwanauchumi).

  1. ‘A trailblazer’: political leaders pay tribute to Madeleine Albright, gazeti la Guardian, UK tar. 23.03.2022 kuhusu maisha yake; hapo jibu lake kuhusu vifo vya watoto nchini Iraki kutokana na vikwazo
  2. Idadi ya watoto waliokufa kutokana na vikwazo inajadiliwa kati ya wataalamu; idadi zilizotajwa na UNICEF (Iraq Child and Maternal Mortality Survey (ICMMS) 1999) hazilingani na data za "UN Inter‑Agency Group on Child Mortality Estimation"
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Madeleine Albright kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.