Tido Mhando
Tido Dustan Mhando ndio jina lake kamili. Mzaliwa wa Muheza mkoa wa Tanga, kabila: Mbondei. Taaluma yake hasa ni Uandishi wa habari na kuwa ni mmoja wa wakongwe wa habari si tu nchini Tanzania bali katika bara la Afrika kwa ujumla. Kwa sasa ni mkurugenzi wa Azam TV.
Tido Mhando anaheshimika nchini Tanzania kwa uzoefu wake mkubwa wa masuala ya habari aliojijengea kwa utumishi uliotukuka kwa miaka mingi ndani ya taaluma yake, uliopelekea hata kufika ngazi ya kuwa mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Habari la BBC.
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Alianzia redio ya taifa, Radio Tanzania Dar Es Salaam, kabla ya kuelekea Kenya ambako alifanya kazi kwa miaka mingi kabla ya kujiunga na shirika la utangazaji la Uingereza, BBC katikati ya miaka ya 1990.
Baada ya kuhamishia makazi yake London nchini Uingereza, Tido Mhando alipewa majukumu ya ukuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC mwaka 1999. Katika muda wake madarakani, Idhaa ya Kiswahili imepata mafanikio makubwa, ikiwa ni pamoja na idadi ya wasikilizaji kupanda mpaka milioni 19 katika ukanda wa Afrika ya Mashariki.
Mzee Tido aliamua kustaafu mwishoni mwa mwezi Oktoba 2006, na kurejea nyumbani Tanzania, ambapo amekuwa akigawa uzoefu wake kwa vijana wa nyumbani kupitia Azam Media Group, kituo anachokiongoza kwa sasa.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Tido Mhando kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |