Nenda kwa yaliyomo

Tido Mhando

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Tido Dustan Mhando (ndilo jina lake kamili; alizaliwa Muheza, mkoa wa Tanga, kabila: Mbondei) ni mshauri wa rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan upande wa habari na mawasiliano kuanzia tarehe 19 Novemba 2025 [1].

Huyo mwandishi wa habari ni mmoja wa wakongwe wa habari, si tu nchini Tanzania bali katika bara la Afrika kwa ujumla. Tido Mhando anaheshimika kwa uzoefu wake mkubwa wa masuala ya habari aliojijengea kwa utumishi uliotukuka kwa miaka mingi ndani ya taaluma yake, uliopelekea hata kufika ngazi ya kuwa mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Habari la BBC. Mwishoni alikuwa mkurugenzi wa Azam TV.

Alianzia redio ya taifa, Radio Tanzania Dar Es Salaam, kabla ya kuelekea Kenya ambako alifanya kazi kwa miaka mingi kabla ya kujiunga na shirika la utangazaji la Uingereza, BBC katikati ya miaka ya 1990.

Baada ya kuhamishia makazi yake London nchini Uingereza, Tido Mhando alipewa majukumu ya ukuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC mwaka 1999. Katika muda wake madarakani, Idhaa ya Kiswahili imepata mafanikio makubwa, ikiwa ni pamoja na idadi ya wasikilizaji kupanda mpaka milioni 19 katika ukanda wa Afrika ya Mashariki.

Tido aliamua kustaafu mwishoni mwa mwezi Oktoba 2006, na kurejea nyumbani Tanzania, ambapo amekuwa akigawa uzoefu wake kwa vijana wa nyumbani kupitia Azam Media Group.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]