Injili ya Marko : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d roboti Nyongeza: vep:Evangelii Markan mödhe
Mstari 44: Mstari 44:
[[arc:ܟܪܘܙܘܬܐ ܕܡܪܩܘܣ]]
[[arc:ܟܪܘܙܘܬܐ ܕܡܪܩܘܣ]]
[[bar:Evangelium noch Markus]]
[[bar:Evangelium noch Markus]]
[[be:Евангелле паводле Марка]]
[[bg:Евангелие от Марко]]
[[bg:Евангелие от Марко]]
[[bo:༄༅།། མར་ཀུས་བྲིས་པའི་འཕྲིན་བཟང་བཞུགས་སོ།།]]
[[bo:༄༅།། མར་ཀུས་བྲིས་པའི་འཕྲིན་བཟང་བཞུགས་སོ།།]]

Pitio la 07:09, 14 Mei 2012

Agano Jipya

Mwinjilisti Marlo katika Biblia ya malkia Theofanu (mnamo 1000)

Injili ya Marko ni kitabu cha pili katika orodha ya Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo. Huhesabiwa kati ya Injili Ndugu pamoja na Mathayo na Luka.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Yaliyomo yake ni habari za Yesu Kristo tangu kubatizwa kwake na Yohane Mbatizaji hadi ufufuko wake.

Mwandishi na wakati wa kuandikwa

Injili yenyewe hamtaji mwandishi wake.

Papias (mnamo mwaka 130) aliandika ya kwamba Yohane Marko alikuwa mwandishi wa taarifa hii. Huyu Yohane Marko anatajwa katika kitabu cha Matendo ya Mitume kuwa mwenyeji wa Yerusalemu aliyemsindikiza Barnaba na Mtume Paulo kwenye safari yao ya kwanza. Papias alisema pia alikuwa mfasiri wa Mtume Petro aliyesikia jinsi Petro alivyosimulia habari za Yesu.

Baadhi ya wataalamu wa leo wana shaka juu ya huyu Marko kuwa mwandishi kwa sababu Injili yenyewe yaonyesha mwandishi wake hakujua vizuri sana habari za Uyahudi.

Kwa upande mwingine kuna pia mapokeo kuwa Marko huyu hakuwa mwenyeji wa Yerusalemu bali mtu mwenye asili ya Afrika ya Kaskazini aliyehamia Palestina baadaye.

Inaonekana ya kwamba Injili iliandikwa kabla ya maangamizi ya Yerusalemu mwaka 70 kwa sababu hakuna dalili ya kwamba mwandishi alikuwa na habari hii.

Yaliyomo

Yaliyomo ni habari za Yesu Kristo tangu kubatizwa kwake na Yohane Mbatizaji hadi ufufuko wake.

  • Ufunguzi wa Injili (1:1-13)
    • Yohane Mbatizaji (1:2-8)
    • Ubatizo wa Yesu (1:9-11)
    • Kujaribiwa kwa Yesu (1:12-13)
  • Kazi ya Yesu katika Galilaya (1:14-9:50)
  • Kazi ya Yesu katika Yudaea na safari ya kwenda Yerusalemu (10)
  • Kazi ya Yesu katika Yerusalemu na ziara ya Bethania (11 - 13)
  • Kesi dhidi ya Yesu na mauti yake (14 - 15)
  • Ufufuo wake (16)

Kiungo

  • [1] Agano Jipya kwa lugha ya Kiswahili.
Makala hii kuhusu mambo ya Agano Jipya bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Injili ya Marko kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.