Lambo la Kihansi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Kigezo:Infobox dam Lambo la Kihansi linapatikana katika mkoa wa Iringa na linapelekea kuundwa kwa bwawa la maji litumikalo kuzalisha umeme nchini Tanzania.

Bwawa la Kihansi lina uwezo wa kuzalisha umeme mpaka kufikia megawatts 180 (241,384 hp) ambapo linachangia asilimia 13 ya umeme unaozalishwa nchini Tanzania [1].

Kwa ujumla[hariri | hariri chanzo]

Kwa ujumla bwawa la Kihansi ni bwawa linalozalisha umeme kwa njia ya kani mvutano yaani graviti, linamilikiwa na shirika la umeme la Tanzania TANESCO. Lilianza kujengwa mnamo Julai 1995 na kukamilika, kisha kufunguliwa na Rais wa awamu ya tatu wa Tanzania, Benjamin W. Mkapa tarehe 10 Julai 2000. Ujenzi wa bwawa la Kihansi umegharimu kiasi cha dola za Kimarekani milioni 275 [1][2][3].

Mahali[hariri | hariri chanzo]

Bwawa la Kihansi, ambalo limetokana na lambo hilo, linapatikana kusini mwa Tanzania kukatisha mto Kilombero katika korongo la Kihansi baada ya kukutana na mto ulanga. Kutoka Dar es Salaam inakadiriwa kuwa ni kilometa 643 kusini[4], wakati kutoka Iringa inakadiriwa ni kilometa 168 kusini, mpakani mwa Wilaya ya Mufindi na Wilaya ya Kilombero[5].

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 Power Technology (2020). Lower Kihansi Hydropower Project. Power-Technology.com.
  2. Myrvoll, Frank (2003). in Frank Myrvoll: Field Measurements in Geomechanics. Taylor & Francis, 245–254. ISBN 978-90-5809-602-- 9. [dead link]
  3. Pierre Julien and Seema Shah (1 November 2005). Sedimentation Initiatives in Developing Countries (Archived from the original on 26 July 2011) 29–31. UNESCO. Jalada kutoka ya awali juu ya 2011-07-26. Iliwekwa mnamo 2020-09-18.
  4. Kigezo:Google maps
  5. Kigezo:Google maps

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Flag-map of Tanzania.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Iringa bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Lambo la Kihansi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.