Konrado wa Piacenza
Konrad wa Piacenza (jina lake kwa Kiitalia lilikuwa Corrado Confalonieri), ambaye alizaliwa Piacenza, Emilia-Romagna, Italia, 1290 hivi, akafariki Noto, Siracusa, Sicilia, Italia visiwani tarehe 19 Februari 1351, alikuwa mkaapweke wa Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko anayeheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu tangu mwaka 1625.
Sikukuu yake huadhimishwa katika tarehe ya kifo chake.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Konrad alizaliwa katika moja ya familia maarufu zaidi ya mji wa Piacenza, akamuoa Efrosina akiwa kijana sana, akiendelea na maisha ya tabaka lake pamoja na kuzingatia dini ya Ukristo.
Kisha mwenyewe kusababisha bila makusudi uharibifu mkubwa kwa moto, mkulima aliyepita huko alikamatwa, akateswa na kisha kulazimishwa kukiri kosa asilolifanya akahukumiwa kufa.
Alipomuona anapelekwa kuuawa, Konrad alikiri kosa lake, na kama fidia alilazimika kuuza maali yake yote.
Yeye na mke wake walioona mkono wa Mungu katika tukio hilo, wakakubaliana kutengana ili kutawa, mmoja mahali pa upweke pa Wafransisko wa Utawa wa Tatu, mwingine katika monasteri ya Waklara.
Mapema alijulikana kwa utakatifu, hivi kwamba umati wa watu waliomtembelea ulimzuia asifaidike zaidi na maisha ya upwekeni aliyojitafutia.
Hapo alifika Roma, na kutoka huko akahamia Noto, Sicilia, alipoishi upwkeni kwa miaka 36 kwa toba kali, akitenda miujiza mingi hadi kifo kilipomkuta akiwa anasali mbele ya sanamu ya Yesu msalabani.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Catholic Encyclopedia: "St. Conrad of Piacenza"
- Saints.Spqn.com
- Saint of the Day Archived 3 Februari 2013 at the Wayback Machine.