Kolo Toure
Youth career | |||
---|---|---|---|
2000–2002 | ASEC Mimosas | ||
Senior career* | |||
Miaka | Timu | Apps† | (Gls)† |
2002–2009 | Arsenal | 225 | (9) |
2009– | Manchester City | 14 | (1) |
Timu ya Taifa ya Kandanda‡ | |||
2000– | Côte d'Ivoire | 70 | (2) |
* Senior club appearances and goals counted for the domestic league only and correct as of 09:12, 15 Desemba 2009 (UTC). † Appearances (Goals). |
Kolo Habib Toure (alizaliwa 19, Machi, 1981), ni mchezaji wa kandanda ambaye kwa sasa anaichezea, na ni nahodha wa Manchester City,ambayo ni klabu ya ligi kuu ya Uingereza na huichezea timu ya taifa ya Ivory Coast. Touré ni mchezaji wa kati wa safu ya ulinzi, yaani difenda, na anajulikana kwa kasi yake, nguvu yake na uanaspoti wake. Yeye ni kaka mkubwa wa Yaya Toure, mchezaji wa kiungo cha kati katika klabu ya Barcelona na Ibrahim Touré wa klabu ya Al-Ittihad.
Wasifu wa Klabu
[hariri | hariri chanzo]Arsenal
[hariri | hariri chanzo]Alizaliwa katika sehemu ya Bouaké, na baada ya jaribio wa muda mfupi, Toure alijiunga na Arsenal mnamo Februari 2002 kutoka ASEC Mimosas kwa paundi £ 150,000. Alipata kibali cha kazi cha Uingereza kutokana na status yake ya kuwa mchezaji wa kimataifa aliyekamilika. Awali alichezeshwa kama mchezaji wa kiungo cha kati wa kushambulia au kama mshambuliaji.
Msimu wa 2002-03
[hariri | hariri chanzo]Toure hakuichezea timu ya kwanza ya Arsenal hadi msimu uliofuata, dhidi ya Liverpool katika FA Community Shield mwezi Agosti mwaka wa 2002. Awali alijulikana kama mchezaji anayeweza kucheza katika sehemu yoyote ya uwanja. Alianza wasifu wake wa Arsenal kama mchezaji wa kiungo cha kati na vilevile kama mchezaji wa safu ya ulinzi wa kulia. Alifunga bao lake la kwanza la Arsenal katika uwanja wa Stamford Bridge dhidi ya Chelsea, mechi iliyokamilika kwa sare ya 1-1. Arsenal ilishindwa kuhifadhi taji lao la Premiership msimu huo, hata hivyo Touré aliweka hatua kubwa katika wasifu wake kwa kushinda kombe la FA Cup.
Msimu wa 2003-04
[hariri | hariri chanzo]Msimu wa 2003-04 ulipoanza, Wenger alianza kumtumia Touré katika kati ya safu ya ulinzi sambamba na Sol Campbell. Wawili hawa walifomu ushirikiano mzuri,na wakawa na msimu mzuri wakati Arsenal ilimaliza msimu mzima bila kushindwa. Yeye, ambaye awali alikuwa mchezaji wa kiungo cha kati wa kushambulia au mshambuliaji, alijitengenezea sifa kwa kuwa mchezaji wa safu ya ulinzi anayeshambulia, na alifunga bao moja na alikuwa na pasi moja iliyosababisha bao; alikuwa na shauku sana kwa mbio zake na kutoka kwa "set-pieces".
Msimu wa 2004-05
[hariri | hariri chanzo]Touré alikuwa ndani na nje ya timu ya Arsenal wakati wa msimu wa 2004-05, kwani alikuwa anapigania nafasi katika timu ya kwanza pamoja na Phillipe Senderos na Pascal Cygan ambao pia walitaka kucheza sambamba na Sol Campbell katika safu ulinzi. Toure alimaliza msimu huo na medali ya kombe la FA na aliicheza Arsenal mechi 50 pamoja na kufunga bao moja. Bao lake la kipekee la msimu wa 2004-05 lilifungwa dakika ya 90 katika mechi ya raundi ya 16 ya kombe la mabingwa barani Ulaya dhidi ya Bayern Munich ya Ujerumani. Arsenal ilipoteza mechi hiyo 3-1.
Msimu wa 2005-06
[hariri | hariri chanzo]Toure alijiimarisha kwa haraka kama mmoja wa wachezji bora wa safu ya ulinzi katika ligi kuu ya Uingereza. Alijiimarisha kama mchezaji wa kudumu katika timu ya kwanza ya Arsenal na pia kama mpenzi kwa washabiki. Katika msimu huu wa 2005-06, aliimarisha ushirikiano wa safu ya ulinzi pamoja na Philippe Senderos. Wawili hawa walikuwa na fomu Imakulata msimu huo ukielekea kuisha kwani waliisaidia timu ya Arsenal kufika fainali ya kombe la mabingwa barani Ulaya la mwaka wa 2006 baada ya Arsenal kutofungwa bao kwa mechi 10 mfululizo (rekodi ya Ulaya ya ushindani). Baada ya maonyesho yake ya kishujaa katika ligi ya mabingwa barani Ulaya, sifa yake ilipanda maradufu, kwani alikuwa sasa anaonekana kama mmoja wa wachezaji bora wa safu ya ulinzi duniani katika nafasi yake. Waandishi wa habari wa Kiitaliano hata walimwita Toure " Fabio Cannavaro wa Afrika" wakati Arsenal iliibandua Juventus nje ya shindano hilo. Toure alionekana kwa upana kama mmoja wa wachezaji wa safu ya ulinzi bora duniani baada ya maonyesho yake na mchezo wake katika kombe la mabingwa barani Ulaya mwaka wa 2006.
Toure alifunga bao lake la pili la Ulaya tarehe 19 Aprili 2006, bao muhimu la ushindi katika nusu fainali ya kwanza ya ligi ya Mabingwa barani Ulaya dhidi ya Villarreal CF. Bao hili lilikuwa bao la mwisho la Ulaya kufungwa katika uwanja wa Highbury na pia lilikuwa bao lililoamua kwa ufanisi nusu fainali hii (Arsenal ilishinda 1-0 kwa jumla), na kuipeleka Arsenal katika fainali yake ya kwanza ya ligi ya Mabingwa barani Ulaya katka mji mkuu wa Paris, Ufaransa.
Msimu wa 2006/07
[hariri | hariri chanzo]Toure alipewa jesi la namba 5 kwa msimu wa 2006-07, ambalo halikuwa limetumiwa tangu kuondoka kwa Martin Keown. Toure alisaini mkataba mpya wa miaka minne na Arsenal ambao thamani yake ilikuwa karibu paundi (£) elfu 70 kwa wiki. Touré alisema "Najiona nikikaa hapa [Arsenal] kwa muda wote wa wasifu wangu" . "Kwa nini nataka kuondoka? Naipenda kandanda yangu hapa, familia yangu inaishi hapa, na klabu hii ina lengo ' Licha ya Arsenal kuwa na kampeni iliyosikitisha, Touré alikuwa thabiti kama kawaida, na alikuwa katika nafasi ya tatu chuma ya Gilberto Silva na Cesc Fabregas katika tuzo la Mchezaji bora wa Arsenal wa msimu.
Msimu wa 2007/08
[hariri | hariri chanzo]Touré alikuwa makamu mdogo wa nahodha katika msimu wa 2006-07 baada ya makamu wa nahodha wa zamani Gilberto Silva na nahodha wa zamani Thierry Henry. Alikuwa nahodha wa Arsenal kwa mara ya kwanza tarehe 9 Januari 2007 katika ushindi wa 6-3 dhidi ya Liverpool katika kombe la Carling. Aliongoza Gunners katika fainali ya shindano hili la kombe la Carling na pia alikuwa nahodha wa Arsenal katika nusu fainali ya kwanza dhidi ya Tottenham Hotspur. Akawa mwanachama wa sasa aliyeitumikia kikosi cha Arsenal kwa muda mrefu kufuatia kuondoka kwa Jeremie Aliadiere, Thierry Henry na Freddie Ljungberg katika dirisha dogo la uhamisho la wakati wa majira wa mwaka wa 2007. Pia alikuwa nahodha wa Arsenal katika msururu wa michezo mapema katika msimu wa 2007-08 baada ya nahodha William Gallas kujeruhiwa katika mechi dhidi ya Blackburn Rovers. Alikuwa na kampeni nyingine muruwa wa 2007-08, kwani alifomu ushirikiano fanisi na mchezaji mwenzake wa safu ya ulinzi, William Gallas. Alifunga "free kick" katika mechi dhidi ya Bolton Wanderers, ambapo shoti yake ya risasi ilipita chini ya wachezaji wa Bolton na kumpita mlinda langa wa Bolton, Jussi Jääskeläinen. Hata hivyo, wakati wa Kombe la Mataifa ya Afrika, yeye alipata jeraha na hakucheza vizuri alilporudi rudi. Kisha akajijeruhi tena katika kombe la mabingwa barani Ulaya dhidi ya AC Milan wakati alilikinga shoti la Alexandre Pato kutumia mguu wake, na alitolewa uwanjani ndiposa apate matibabu zaidi. Toure alirejea katika timu ya kwanza dhidi ya Middlesbrough tarehe 15 Machi na alifungia Arsenal bao la kusawazisha katika dakika 10 za mwisho. Katika robo fainali ya kombe la mabingwa barani Ulaya, alicheza upande wa kulia wa safu ya ulinzi ambao haifahamu vyema, mechi ambayo Arsenal walikuwa wanatoka sare ya 2-2 na Liverpool. Lakini, katika dakika ya 86, Toure ilihukumiwa kwa kumsukuma Ryan Babel katika boksi ya penalti. Arsène Wenger, hata hivyo, alimtetea Touré, kwa kusema kuwa refari alifanya uamuzi mbaya. Steven Gerrard aliichapa penalti hiyo na kutikisa wavu. Mechi hiyo ilikamilika 4-2, ushindi ukiwa wa Liverpool kutokana na bao la Babel wakati wa muda wa ziada.
Msimu wa 2008/09
[hariri | hariri chanzo]Tarehe 1 Januari 2009, Toure alidai kuwa alitaka kuihama Arsenal baada ya ugomvi baina yake na mchezaji mwenzake wa safu ya ulinzi William Gallas. Iliripotiwa kuwa alitoa ombi la uhamisho ambalo baadaye lilikataliwa na mwenyekiti wa Arsenal, Peter Hill-Wood. Hata hivyo, Touré alibadilisha uamuzi wake kwa muda mfupi na kuonyesha nia yake ya Gunners angalau hadi msimu ulipokamilika.
Manchester City
[hariri | hariri chanzo]Msimu wa 2009/10
[hariri | hariri chanzo]Baada ya uvumi mwingi wa uhamisho, ilitangazwa mnamo 28 Julai 2009 kwamba Manchester City ilikubali kumnunua Kolo Toure kwa ada ya paundi (£) milioni 14. Baada ya kufanikiwa kupita kwa matibabu katika Manchester tarehe 29 Julai 2009, Toure alisaini mkataba wa miaka minne Manchester City ambayo ina chaguo la kuendeleza kwa zaidi ya miaka 5. Manchester City, ambayo ilimaliza katika nafasi ya 9 msimu uliyopita, ilikuwa imewatia saini wachezji wa kiwango cha juu katika maandalizi kwa msimu wa 2009-10, na Touré anatarajia kuisaidia City kuwa katika nafasi moja ya nne za kwanza ya ligi kuu ya Uingereza. Hivi karibuni aliteuliwa kuwa nahodha wa klabu hiyo na meneja wa hapo awali, Mark Hughes. Alifunga bao lake la kwanza la Manchester City katika ushinda wa 2-1 dhidi ya Fulham tarehe 23 Septemba 2009 katika mechi ya Kombe la Carling. Alifunga bao lake la kwanza la ligi la Manchester City dhidi ya Burnley tarehe 7 Novemba 2009.
Wasifu wa Kimataifa
[hariri | hariri chanzo]Toure ameichezea nchi ya Cote d'Ivoire tangu mwaka wa 2000. Mechi yake ya kwanza ilikuwa mnamo Aprili 2000 dhidi ya Rwanda. Yeye ni chaguo la kwanza la mchezaji wa kati katika safu ya ulinzi. Alicheza mechi zote tano za Cote d'Ivoire lakini walibanduliwa nje ya Kombe hilo na wenyeji Misri mnamo Januari 2006.
Alitajwa katika kikosi cha watu 23 kilichochukuliwa na kocha Henri Michel kwenda kushiriki katika kombe la dunia la mwaka wa 2006 na alicheza mechi yake ya kwanza katika Kombe la Dunia tarehe 11 Juni 2006, mechi ambayo Cote d'Ivoire ilipoteza 1-2 dhidi ya Ajentina. Ameifungia Ivory Coast mabao mawili kwa mechi sabini alizozichezea hadi sasa, yote kutumia kichwa dhidi ya Gabon (Nyumbani) na Tajikistan (Ugenini) mtawalia.
Mabao ya kimataifa
[hariri | hariri chanzo]# | Tarehe | Ukumbi | Mpinzani | Mabao | FT Result | Mashindano | ||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|
1 | 8 Oktoba 2002 | Abidjan, Ivory Coast | Gambia | 3 -0 | 5-0 (Win) | 2008 Afrika ya Kombe la Mataifa ya kufuzu | ||
2 | 25 Juni 2003 | Dushanbe, Tajikistan | Tajikistan | 1-2 | 1-8 (Win) | Maonyesho mchezo |
Mbinu ya kucheza
[hariri | hariri chanzo]Touré anajulikana kwa kasi na nguvu yake, ambazo humwezesha kuwatoa washambulizi dhaifu kutoka kwa mpira na kupambana na washumbilizi wenye mbio. Ana uwezo mzuri wa kumshika mpinzani na makabiliano mengi huwa wa wakati muafaka nah hii imechangia rekodi yake nzuri ya nidhamu. Ingawa ni mfupi kama mchezaji wa kati wa safu ya ulinzi, yeye huruka juu sana.
Takwimu ya Wasifu
[hariri | hariri chanzo]- (Correct kama ya 25 Agosti 2009)
Club | Season | League | Cup* | Europe | Total | ||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Apps | Goals | Assists | Apps | Goals | Assists | Apps | Goals | Assists | Apps | Goals | Assists | ||
Arsenal | 2002–03 | 26 | 2 | 1 | 7 | 0 | 0 | 7 | 0 | 0 | 40 | 2 | 1 |
2003–04 | 37 | 1 | 1 | 8 | 2 | 0 | 10 | 0 | 0 | 55 | 3 | 1 | |
2004–05 | 35 | 0 | 0 | 7 | 0 | 0 | 8 | 1 | 0 | 50 | 1 | 0 | |
2005–06 | 33 | 0 | 0 | 1 | 0 | 0 | 12 | 1 | 1 | 46 | 1 | 1 | |
2006–07 | 35 | 3 | 3 | 8 | 1 | 1 | 10 | 0 | 0 | 53 | 4 | 4 | |
2007–08 | 30 | 2 | 3 | 2 | 0 | 1 | 9 | 0 | 0 | 41 | 2 | 4 | |
2008–09 | 29 | 1 | 1 | 3 | 0 | 0 | 9 | 0 | 0 | 41 | 1 | 1 | |
Total | 225 | 9 | 9 | 36 | 3 | 2 | 65 | 2 | 1 | 326 | 14 | 12 | |
Manchester City | 2009–10 | 14 | 1 | 0 | 2 | 1 | 0 | 0 | 0 | 0 | 16 | 2 | 1 |
Jumla | 14 | 1 | 0 | 2 | 1 | 0 | 0 | 0 | 0 | 16 | 2 | 1 | |
Career total | 239 | 10 | 9 | 38 | 4 | 2 | 65 | 2 | 1 | 342 | 17 | 13 |
(* FA Cup, Kombe la Carling na Community Shield)
Maisha ya Kibinafsi.
[hariri | hariri chanzo]Kolo Toure ni Mwislamu. Yeye ni kakaze wa Yaya Toure wa FC Barcelona na Ibrahim Touré ambaye ni mshambuliaji wa Al-Ittihad.
Tuzo
[hariri | hariri chanzo]Mimosas
[hariri | hariri chanzo]- Côte d'Ivoire Premier Division: 2001, 2002
Arsenal
[hariri | hariri chanzo]Mshindi
- FA Premier League: 2003-04
- Kombe la FA: 2007, 2009
- FA Community Shield: 2002, 2004
Nafasi ya pili
- Ligi kuu ya Mabingwa barani Ulaya : 2005-06
- Ligi kuu ya Uingereza: 2002-03, 2004-05
- Kombe ya Carling:2003
- FA Community Sheld (2): 2003, 2005
Kimataifa
[hariri | hariri chanzo]Nafasi ya pili
- Kombe la Mataifa ya Afrika: 2006
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Profile Archived 17 Desemba 2008 at the Wayback Machine. saa Arsenal.com
- Kolo Touré career stats kwenye Soccerbase
- Stats na photos saa Sporting Heroes