Vincent Kompany

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Vincent Kompany akiwa mazoezini.

Vincent Jean Kompany (alizaliwa 10 Aprili 1986) ni mchezaji wa soka wa Ubelgiji ambaye anacheza kama beki katika klabu ya Uingereza Manchester City na timu ya taifa ya Ubelgiji.

Katika msimu wa 2011-12 alipewa unahodha katika klabu ya Manchester City, akiongoza klabu yake kushinda Ligi Kuu ya msimu huo Yeye pia ni mwenyekiti wa Belgium D3B Division.

Kompany alianza kazi yake huko Anderlecht, alitumia miaka mitatu katika klabu hiyo ya Ubelgiji kabla ya kwenda katika klabu ya Bundesliga Hamburg mwaka 2006. Katika majira ya joto ya 2008, akiwa na umri wa miaka 22, alimaliza na kuhamia Manchester City.


Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Vincent Kompany kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

.