Kolekta
Mandhari
Kolekta (kutoka Kilatini collēcta[1][2] ambayo ni sawa na Kigiriki [déesis] synapté; kwa Kiingereza collect[3]) ni sala fupi ya liturujia ya madhehebu mbalimbali ya Ukristo, kama yale ya Wakatoliki, Waorthodoksi, Waanglikana, Wamethodisti na Walutheri.
Tafsiri ya jina la Kilatini collēcta (kutoka kitenzi colligō, "kukusanya") ni mkusanyiko wa waumini au zaidi ni mkusanyo wa maombi ambayo kila muumini ametoa binafsi wakati wa kimya ambao padri anauacha kati ya mwaliko wa kusali ("Tuombe") na sala anayoitamka mwenyewe akiitikiwa na wote, "Amina"[1][2].
Katika Misa ya Kanisa la Kilatini sala hiyo inafunga ibada za kuanzia na inafuatwa na liturujia ya Neno.
Muundo
[hariri | hariri chanzo]Kwa kawaida kolekta ina sehemu tano:[1][4]: 250
- Mwelekeo, yaani nafsi ya Kimungu ambaye anaombwa (Mungu Baba, mara chache Mungu Mwana
- Sifa ya nafsi hiyo, mara nyingi kuhusiana na ombi litakalofuata
- Ombi la kitu kimoja kwa namna wazi[4]: 249
- Lengo la ombi:
- Hatima inayomhusisha Yesu Kristo na kumaliziwa na waumini.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 1.2 C. Frederick Barbee, Paul F.M. Zahl, The Collects of Thomas Cranmer (Eerdmans 1999 ISBN 9780802838452), pp. ix-xi
- ↑ 2.0 2.1 "Edward McNamara ZENIT liturgy questions, 28 August 2012". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-08-30. Iliwekwa mnamo 2017-10-05.
- ↑ Foley, Edward (2011). A Commentary on the Order of Mass of the Roman Missal. Liturgical Press. uk. 141. ISBN 9780814662472.
- ↑ 4.0 4.1 Fortescue, Adrian (1914). The Mass: A Study of the Roman Liturgy (tol. la 2nd). Longmans, Green and Co.
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kolekta kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |