Amina

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
“Amina”
“Amina” cover
Kava la Amina
Single ya Sanaipei Tande
Imetolewa 2017
Muundo Upakuzi mtandaoni
Imerekodiwa 2017
Aina Afropop, Muziki wa dunia
Urefu 3:36
Studio House of Dillie
Mtunzi Sana
Mtayarishaji House of Dillie
Mwenendo wa single za Sanaipei Tande
"Your Property"
(2016)
"Amina"
(2017)

"Amina" ni jina la wimbo uliotoka mwaka 2017 wa msanii wa muziki wa afropop kutoka nchini Kenya - Sanaipei Tande.

Wimbo umetayarishwa na House of Dillie kwa maudhui ya kusikitisha ili kusindikiza midundo ya ndani. Ni moja kati ya nyimbo za huzuni sana kwa mwaka 2017. Sana ameonesha uwezo wa hali ya juu katika uimbaji tangu akiwa na bendi ya Sema hapo 2004/2005. Lakini kadiri anavyozidi kwenda mbele ndivyo uwezo unazidi kutamalaki. Wimbo umeonekana kuzungumzia maisha yake na usia kwa wasichana wasikate tamaa katika utafutaji wa maisha. Maisha yana mambo mengi, furaha, huzuni, matumaini, kusameheana, urafiki na kadhalika. Alitendwa kimahaba, hisia zake kaamua kuziweka katika wimbo.[1]

Dhumuni la wimbo huu hasa ni kumuimbia binamu yake aliyefariki katika ajali ya gari akiwa anaelekea Mombasa kuposwa. Kupitia majonzi yake aliweza kutunga wimbo wa kuenzi uhusiano wao.[2]

Maudhui[hariri | hariri chanzo]

Ubeti wa kwanza[hariri | hariri chanzo]

Sampuli ya "Amina" ubeti wa kwanza na kiitikio.

Maudhui ya wimbo kwa baadhi ya mistari inayopatikana katika wimbo;

Ubeti wa kwanza anamwomba msamaha mamake mzazi kwa matendo ya ujana. Ujana una mambo kiasi hata hupelekea wazazi kukereka na miyenendo ya watoto zao.

Tazama:

"Ooh mama, panguza chozi

Siyatafakari vita vya juzi

Si kupenda kwangu kukuudhi

Ila tu ujana haubagu"

Vilevile kuvumilia maneno ya wanadamau. Uzushi mwingi usikufanye ukonde kwa maneno ya wanadamu. Wanadamu wamelizaliwa wanasema.

Rudia mstari:

"Dada panguza chozi

Sijitie lawama kwa uzushi

Kwani vita kati ya mandugu si ya firauni"

Kipande cha tatu anaielezea nafasi iliyoaga dunia. Wapo watakaokusema kwa mabaya ungali maiti, kipindi hiki si chema kumsema mtu mabaya yake. Tujitahidi kutubu na kuishi na watu vizuri tukiwa hai, kwani ukifikwa na umauti huna utakaloweza muda ushakupita.

Rejea mistari:

"Wakati hauniruhusu mi

Kurekebisha yangu madhambi

Kwa hivyo nawaomba siku hii

Nikumbukie mazuri"

Halafu anagusia kidogo ile tabia ya misibani kulia, yeye kwake anataka watu wacheke badala ya kulia. Hataki marafiki zake wawe wapweke ilhali yupo hai na kwa pamoja tuishi kwa furaha na upendo.

Rejea mistari hii:

"Mi nataka mucheke siku ya mwisho

Siwe mpweke mi bado niko

Namshukuru Mola kwa kuwepo

Nasema Amina"

Halafu anaimba kiitikio kwa kumshukuru Mola wetu kwa pumzi na yote aliyotujaalia kwa kusema:

"Amina amina A A amina

Amina amina A A amina

Amina amina A A amina

Amina amina"

Ubeti wa pili[hariri | hariri chanzo]

Ubeti wa pili hasa umelenga kuhasa vijana wenzake wapunguze mawazo pindi wanapopata shida katika maisha. Matatizo maishani ni jambo la kawaida, yakikufika, shukuru Mungu na jitahidi kukabiliana kadiri uwezavyo. Ukitendwa, usichukie kiasi moyo ukajawa na fundo, hata ukisema hupendi tena, haisaidi kwani hasira hasara. Raha na karaha vyote vinatoka kwa muumba.

Rejea mistari.

"Ooh mpenzi panguza chozi

Sijijaze chuki wewe moyoni

Hasira hasara

Yote ya mwenyezi

Oh rafiki panguza chozi

Sijiumize we kichwa na maswali

Utansamehe sana kwenda bila mkono wa buriaani"

Vilevile anazungumzia misimamo thabiti katika mapenzi hasa kwa wale waliokuumiza. Hakuna mwanadamu asiye na jema, licha ya mateso aliyompa, bado aliendelea kukumbuka mazuri yake, ila tu, hawezi tena kuwa nae.

"Ooh sina sina sina sina

Nafasi nyingine, Ya kuwa na wewe

Nasikitika mi naumia

Lakini nina nina nina nina

Shukrani moyoni, yakuwa miongoni

mwa walo nienzi mi"

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]