Kizito

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Dirisha la kanisa la Namugongo linaloonyesha Mt. Kizito.
Mt. Kizito akibatizwa na Mt. Karolo Lwanga huko Munyonyokioo cha rangi katika patakatifu pa wafiadini huko Munyonyo.

Mtakatifu Kizito (1872 - Namugongo, Uganda, 3 Juni 1886) ni mmojawapo wa Wafiadini wa Uganda, mdogo kuliko wote.

Alichomwa moto kwa ajili ya imani yake kwa Yesu Kristo akiwa na umri wa miaka 14 tu. Kidogo tu kabla hajauawa alibatizwa na katekista Karolo Lwanga.

Pamoja na wenzake alitangazwa na Papa Benedikto XV kuwa wenye heri tarehe 6 Juni 1920, halafu na Papa Paulo VI kuwa mtakatifu tarehe 18 Oktoba 1964 huko Roma.

Sikukuu yake ni tarehe 3 Juni kila mwaka[1].

Ni msimamizi wa watoto na wa shule za msingi.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • J. FRANSE, W.F., Mashahidi 22 wa Uganda – tafsiri ya C. Kuhenga n.k. – ed. T.M.P. Book Department – Tabora 1981

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.