Kikyrili

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Kikyrili ni aina ya mwandiko au alfabeti inayotumiwa kuandika lugha mbalimbali za Ulaya ya Mashariki na Asia ya Kati kwa mfano Kirusi, Kiserbia, Kitajiki. Jina limetokana na mmonaki na mtalaamu Mgiriki Mt. Kyrilo (827 - 14 Februari 869) aliyesemekana aliunda namna ya mwandiko kwa ajili lugha za Kislavoni pamoja na mwenzake Mt. Methodio.

Mwandiko kwa ajili ya lugha za Kislavoni[hariri | hariri chanzo]

Hali halisi hawakuanzisha aina hii ya alfabeti lakini waliendeleza namna ya kuiandika iliyosaidia kusambaza mwandiko kati ya mataifa wasemaji wa lugha za Kislavoni. Lugha hizi zina sauti kadhaa ambazo hazina herufi katika alfabeti ya Kilatini. (Mwandiko wa Kilatini hutumiwa siku hizi kwa lugha nyingi duniani pia Kiswahili na wikipedia hii.)

Kuna lugha za Kislavoni kama vile Kipoland, Kiceki, Kikroatia zinazoandikwa kwa alfabeti ya Kilatini lakini hapo kuna alama za nyongeza kwa ajili ya sauti za pekee za lugha za Kislavoni kwa mfano: "Č" kwa sauti ya "tsh" au "Ž" kwa aina ya "sh laini".

Alfabeti za Kikyrili zinatofautiana kiasi kati ya lugha na lugha; kuna namna tofauti za kuandika sauti ileile au pia herufi za pekee kwa ajili ya sauti za pekee katika lugha fulani. Alfabeti inayotumiwa na watu wengi ni ya Kirusi inayoonyeshwa hapa.

Lugha za Kislavoni zinazoandikwa kwa alfabeti ya Kikyrili ni:

Mwandiko wa lugha za Kiasia[hariri | hariri chanzo]

Kutokana na athira ya Urusi katika Asia ya kati kuna pia lugha mbalimbali za Kiasia ambazo zinaandikwa kwa mwandiko wa Kikyrili tangu karne ya 19 au mwanzo wa karne ya 20. Nchi zinazohusu zilikuwa ama sehemu za Umoja wa Kisovyet au nchi jirani kama Mongolia.

Lugha kadhaa za Kiasia zinazoandikwa siku hizi kwa alfabeti za Kikyrili ni:

  • Kikazakhstan
  • Kikirgizistan
  • Kimari
  • Kimongolia
  • Kitajikistan
  • Kichechenia
  • Kiturkmenistan
  • Kiuzbekistan

Mfano wa alfabeti ya Kirusi[hariri | hariri chanzo]

Herufi za Kikirili
(kubwa / ndogo)
Herufi za Kilatini zinazolingana Matamshi
А а A a a
Б б B b b
В в V v v
Г г G g g (w)
Д д D d d
Е е E e e / ye
Ё ё Ë ë yo
Ж ж Ž ž sh laini
З з Z z z
И и I i i
Й й J j i fupi
К к K k k
Л л L l l
М м M m m
Н н N n n
О о O o o
П п P p p
Р р R r r
С с S s s
Т т T t t
У у U u u
Ф ф F f f
Х х Kh kh kama matamshi ya Kiarabu
"Alkhamisi" (Alhamisi)
Ц ц C c ts
Ч ч Č č tsh
Ш ш Š š sh
Щ щ Ŝ ŝ shtsh
Ъ ъ " (alama gumu) alama hii hunonyesha matamshi
„magumu“ ya herufi inayotanguulia
Ы ы Y y Y y
Ь ь (alama laini) alama hii huonyesha sauti
ya "y" baada ya herufi
Э э È è e fupi
Ю ю Û û yu
Я я Â â ya