Kibelarus
Kibelarus (беларуская мова, "biełaruskaja mova" - lugha ya Kibelarus) ni lugha ya watu wa Belarus ikiwa moja kati ya lugha tatu za Kislavoni cha Mashariki pamoja na Kiukraine na Kirusi. Kibelarus inashirikiana maneno ya lugha hizi, pia imepokea sehemu ya msamiati wake kutoka Kipoland kutokana na historia ndefu ya pamoja kati ya Poland na Belarus. Lugha za Kislavoni ni sehemu ya jamii ya Lugha za Kihindi-Kiulaya.
Kibelarus huandikwa mara nyingi kwa mwandiko wa Kisirili lakini kuna pia namna ya kuiandika kwa mwandiko wa Kilatini.
Idadi ya wasemaji ni kati ya milioni 7 au 8. Kibelarus ni lugha rasmi katika nchi ya Belarus. Kuna pia wasemaji nchini Poland katika eneo la Białystok) halafu kati ya vikundi vya wahamiaji waliotoka Belarus na kukaa Marekani, Kanada na Australia.
Fasihi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- makala za OLAC kuhusu Kibelarus Archived 26 Desemba 2014 at the Wayback Machine.
- lugha ya Kibelarus katika Glottolog
- http://www.ethnologue.com/language/bel
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kibelarus kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |