Nenda kwa yaliyomo

Kikalio cha Dhahabu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kikalio cha dhahabu)
Kikalio cha Dhahabu kwenye kiti chake cha enzi, hwedom dwa (1935)
Bendera ya Ufalme wa Ashanti inayoonyesha Kikalio cha Dhahabu

Kikalio cha Dhahabu (kwa Kiashanti - Kitwi: Sika Dwa Kofi, "Kiti cha Dhahabu kilichozaliwa Ijumaa"; kwa Kiingereza: Golden Stool) ni kiti cha enzi cha kifalme cha wafalme wa Ufalme wa Ashanti na ishara kuu ya mamlaka kuu. [1] Kulingana na mapokeo, Okomfo Anokye, Kuhani mkuu na mmoja wa waanzilishi wakuu wa ufalme wa Ashanti, alisababisha kikalio hicho kushuka kutoka mbinguni na kutua kwenye paja la Osei Tutu aliyekuwa mfalme wa kwanza wa Ashanti.[2]

Kikalio cha Dhahabu kinaaminika kuwa na roho [3] ya taifa la Ashanti ndani yake.

Mgogoro wa kihistoria

[hariri | hariri chanzo]

Vita nyingi [4] zimeibuka juu ya umiliki wa kiti hicho cha kifalme. [5] Mnamo mwaka wa 1900, Sir Frederick Hodgson, Gavana Mwingereza wa Gold Coast, alitaka [6] kukalia Kikalio cha Dhahabu akaamuru kipelekwe mbele yale. Lakini Waasante walikificha. Ufatwaji wa kiti ulisababisha uasi wenye silaha unaojulikana kama Vita ya Kikalio cha Dhahabu, ambayo ilisababisha maeneo ya Ashanti kutwaliwa na Uingereza na kuwa koloni. Lakini Waingereza walishindwa kupata kiti.

Mnamo 1921, wafanyakazi Waafrika kadhaa waliojenga barabara waligundua kikalio cha dhahabu wakavua mapambo kadhaa ya dhahabu. Walikamatwa na Waingereza, kabla ya kuhukumiwa adhabu ya kifo kulingana na mila ya Ashanti. Waingereza waliingilia kati na badala yake wahukumiwa walifukuzwa katika Ghana. Hapo serikali ya kikoloni iliahidi kwamba haitaingilia tena mambo ya kikalio kikatolewa mafichoni. [7]

Mnamo mwaka wa 1935 kikalio kilitumika katika sherehe ya kumtawaza Osei Tutu Agyeman Prempeh II. [8]

Muonekano na ufundi

[hariri | hariri chanzo]
Kiti cha Waakan kinachofanana na muundo wa Kikalio cha Dhahabu

Kikalio cha Dhahabu ni kiti kilichopindika sm 46 juu chenye nafasi ya upana wa sentimita 61 kwa 30.[9] Uso wake wote umepambwa kwa dhahabu, na umetundikwa na kengele kumwonya mfalme juu ya hatari inayokuja. [10]  ] Haikuonekana na watu wengi, ilhali ni mfalme tu, malkia, na washauri wanaoaminika wanajua maficho yake.

Mifano yake yametengenezwa kwa ajili ya machifu na kwenye mazishi yao hupakwa damu ya wanyama. [11]  ] Kikalio cha dhahabu ni moja ya ishara kuu za Asante leo kwa sababu bado inaonyesha mfululizo wa kifalme na mamlaka. [12]

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Kuhusu kiti kama ishara ya mamlaka: Ukulu mtakatifu

 1. "African Gold-weights in the British Museum".
 2. "How the Asantehene climaxed the 20th anniversary on the Golden Stool [PHOTOS]". www.graphic.com.gh. 2019-04-22. Iliwekwa mnamo 2019-05-18.
 3. Kyerematen, A. (1969). "The Royal Stools of Ashanti". Africa: Journal of the International African Institute. 39 (1): 1–10. doi:10.2307/1157946. ISSN 0001-9720. JSTOR 1157946.
 4. "Golden Stool of the Asante". History of International Relations (kwa American English). 2018-10-14. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-10-28. Iliwekwa mnamo 2020-02-22.
 5. "Asante Art - Artefacts - Stools". asante.neocities.org. Iliwekwa mnamo 2020-02-22.
 6. "History of Golden Stool". www.ghanaweb.com. Iliwekwa mnamo 2020-02-22.
 7. Carmichael, John (1993). African Eldorado - Gold Coast to Ghana. Gerald Duckworth & Co. Ltd. ku. 176–77. ISBN 0-7156-2387-7.
 8. Michael T. Kaufman. "Opoku Ware II, King of Asante, Is Dead at 89", March 4, 1999. 
 9. "How a mysterious Golden Stool is keeping the great Ashanti kingdom united". Face2Face Africa (kwa Kiingereza). 2018-09-20. Iliwekwa mnamo 2020-02-22.
 10. Yussif, Elias (2013-07-24). The Facet of Black Culture (kwa Kiingereza). Trafford Publishing. ISBN 978-1-4669-8848-4.
 11. Hadzija, Boka (Novemba 2013). My Door is Always Open: A Memoir (kwa Kiingereza). Xlibris Corporation. ISBN 978-1-4836-2925-4.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 12. "Asante Art - Artefacts - Stools". asante.neocities.org. Iliwekwa mnamo 2020-02-22.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]